MAANDAMANO KATIKA KILELE CHA SIKU YA SHERIA NCHINI NJOMBE
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.LUTH MSAFIRI AKIWA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE
MAWAKILI WA SERIKALI NA WAKUJITEGEMEA
MAHAKIMU WA MAHAKAMA ZA MWANZO MKOANI NJOMBE
MWAKILISHI WA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MATIKU NYANGERO AKISOMA TAARIFA YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.
MWAKILISHI WA CHAMA CHA MAWAKILI AFRIKA MASHARIKI EDWIN ENOS SWALE AKISOMA TAARIFA YA SHERIA
NJOMBE
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopha Ole Sendeka Amezitaka Mahakama na Vyombo vya Kisheria Kuzingatia wakati wa kushughulikia kesi na kuwa wepesi katika kupokea ,kuchunguza kesi,kuhukumu na kutoa nakala za hukumu kwa wakati na kwamba haki ikitolewa kwa wakati itachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na mtu Binafsi.
Akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopha Ole Sendeka ,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Luth Msafiri amepongeza kwa kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Umuhimu wa Utoaji Haki Kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi na kwamba kauli mbiu hiyo inadhihirisha Umakini,na Weledi wa kuunga mkono kukua kwa kasi na viwango kwa uchumi wa taifa la Tanzania.
Bi.Msafiri amesema kasi hiyo itasaidia kufikia uchumi wa Viwanda ifikapo 2025 ambapo amewaomba wanasheria wa kujitegemea na serikali kutoa mchango wao kwa makusudi ya kusaidia Mhimili wa Mahakama uweze kutimiza jukumu lake la kutafsiri sheria na kutoa haki za wadau katika mashauri mbalimbali kwa kutumia muda mfupi na kwa tija kubwa.
Bi.Msafiri Pia amewaomba wanasheria Mkoa wa Njombe kuzingatia sheria ,Utu, Uaminifu,Uadilifu na uwajibikaji huku akitaka washiriki kupiga vita adui wa haki ambaye ni Rushwa kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vingine ikiwemo Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini Takukuru.
Akitoa taarifa ya mahakama Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Njombe John Kapokoro Amesema jumla ya mashauri 408 hayajamalizika katika mahakama zilizopo kwenye Wilaya za Mkoa wa Njombe na kutaka kushirikiana na mawakili wa serikali, na wakujitegemea kukamilisha mashauri hayo huku Mahakimu nao wakitakiwa kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.
Wakisoma taarifa mbalimbali mawakili wa serikali na kujitegemea akiwemo Mwakilishi wa chama cha mawakili Afrika Mashariki Edwin Swale na Wakili wa serikali Matiku Nyangero wamesema Mahakama inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mashauri kuchelewa kuanza kusikilizwa ,upelelezi kutokamilika na kuathili utoaji wa haki mahakamani.
Baada ya kuhitimisha Hotuba yake mgeni rasmi amelazimika kwenda kusikiliza kesi moja ya Matumizi ya madawa ya kulevya inayowakabili watuhumiwa wawili wakazi wa mtaa wa National Housing Michael Danda na Shakila Mbena ambayo Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Njombe John Kapokoro ameahirisha shauri hilo hadi tarehe 7 mwezi februari mwaka huu itakapokwenda kusikilizwa tena.
Awali Wakili wa Serikali Matiku Nyangero ameiambia Mahakama kuwa Washtakiwa Michael Danda Na Shakira Mbena Wakiwa kama Mke na Mume walikutwa na Kete 96 za bangi nyingine zikiwa chumbani kwao na nyingine zikiwe kwenye Mdori Karibu na mlango wa kuingilia chooni ambapo walikutwa nazo mnamo septemba 26 mwaka 2016.
Hakimu Kapokoro ameahirisha kesi hiyo na itakwenda kusikilizwa tarehe 7 mwezi wa pili mwaka huu kutokana na mashahidi kutokuwepo ambapo ameagiza kuwaandikia kwa samanzi na kuwapelekea mashahidi ili tarehe hiyo waweze kufika kutolea ushahidi wao huku washtakiwa wakiachiwa kwa dhamana .
.........................................................................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment