Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, January 16, 2017

WANANCHI MAKAMBAKO ENEO LA UWANJA WA POLISI WARUHUSIWA KUENDELEA NA UJENZI ENEO WALILOONESHW.



 
 SAFARI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIWA AMEONGOZANA NA WANANCHI NA VIONGOZI WENGINE KWENDA KUANGALIA ENEO ANALONYANYASIKA NA KUONDOLEWA  NA POLISI KWA MADAI NI LA POLISI MWANANCHI HARUHUSIWI KUJENGA IKIWA WENGINE WALIJENGA TANGU MWAKA 1992 HADI LEO WANAISHI NA WANALIPIA KODI HALMASHAURI.
 

KAIM MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO BWANA SALMU MLUMBE AKIFUNGUA MKUTANO MWANZONI KABISA.
MBUNGE WA MAKAMBAKO DEO SANGA  MAARUFU JA PEOPLE AKIZUNGUMZA MACHACHE KUHUSIANA NA ALIVYOTEKELEZA MIRADI YAKE MJINI HAPO.



MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAKAMBAKO.


HOTUBA AKITOA MKUU WA MKOA HUYO OLE SENDEKA KABLA YA KWENDA KAKAGUA MAENEO YANAYOLALAMIKIWA NA WANANCHI.


 MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA  AKIWA AMEONGOZANA NA MBUNGE WA MAKAMBAKO DEO SANGA,MKUU WA WILAYA YA NJOMBE RUTH MSAFIRI,KAIMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO  SALMU MLUMBE NA KATIBU TAWALA WA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAHU.
 WANANCHI HAWAKUKAA MBALI KUSIKILIZA MAAMUZI YA MKUU WA MKOA JUU YA KIWANJA CHA MAMA MJANE PAMOJA NA WALIOJENGA KARIBU NA ENEO ALILOKUWA AKIZUILIWA ASIJENGE MJANE HUYO.
 SASA WANANCHI WANAHOJI HUYU OCD WAKATI KITUO CHA POLISI KINAJENGWA NA NYUMBA HIZO ALIKUWEPO YEYE SI MTUMISHI TU ANAYEPELEKWA KITUO FRANI NA KUHAMISHIWA KITUO KINGINE KWANINI ANG'ANG'ANIE ENEO AMBALO WANANCHI HAWAJAWAHI HATA KULIPWA FIDIA AU KUNA KIGOGO ANATAKA AJIMILIKISHE ENEO HILO?

 OCD WA KITUO CHA POLISI MAKAMBAKO AKIMUONESHA MKUU WA MKOA KWAMBA HAPA PANA BOMBA AMBALO NDILO MPAKA WA MAENEO YA POLISI







NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopha Ole Sendeka amefanikiwa kutatua mgogoro wa viwanja na Nyumba zilizodaiwa kujengwa ndani ya eneo la Polisi Mjini Makambako kwa kuwaruhusu wananchi walio nje ya barabara ya Halmashauri kuendelea kujenga.

Akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa polisi     Makambako Ole Sendeka amesema kuna baadhi ya wananchi waliopo ndani ya Barabara iliyotengwa na halmashauri watatakiwa kulipwa fidia na kutafutiwa eneo lingine la kujenga ili kupisha eneo hilo wanaloishi kwaajili ya Polisi.

Hatua hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopha Ole Sendeka  ya kutoa maamuzi hayo imefuatia mama mmoja ambaye ni mjane kulalamikia  kunyanyaswa na jeshi la polisi makambako kwa kumkamata na kumuweka ndani yeye na mafundi wake pasipo kuwapeleka mahakamani ili apishe eneo analoanza kujenga nyumba yake.
Ole Sendeka amesema halmashauri inatakiwa kuwalipa fidia haraka  wananchi  waliopo ndani ya eneo linalodaiwa la polisi mjini Makambako na kuwatafutia eneo lingine la kujenga ili wananchi ambao walijenga nyumba zao kwa muda mrefu waweze kupisha eneo hilo kwaajili ya shughuli za kipolisi

"Halmashauri hakikisheni mnawalipa fidia haraka wananchi hawa waliopo ndani ya eneo hili na ninyi wananchi mlio nje ya barabara tulioiona ya halmashauri msivuke barabara hiyo endeleeni kujenga nyumba zenu na mama wewe mjane uliyekuwa ukinyanyasika kaendelee kujengab asiwepo mtu yeyote wakuwabughudhi" Amesema Ole Sendeka.

"Ole Sendeka amesema serikali hiyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haipendi kumuonea mtu yeyote inataka kuwatendea haki wananchi wote hakuna cha polisi kumnyanyasa mwananchi na wananchi mukiona mtumishi yeyote anawanyanyasa  nipigieni simu awe polisi,mkurugenzi au mtumishi yeyote yule ataondoka tu atuache na serikali yetu ya Magufuri" Aliongeza Mkuu huyo wa mkoa wa Njombe.

Kwa upande wake kamanda wa polisi Wa Halmashauri ya Mji wa Makambako OCD Peter Kaiza amesema barabara inayotanjwa na Halmashauri pamoja na wananchi kuwa ni mpaka haikuwepo na kutaka wananchi waliojenga eneo hilo kuondoka mara moja jambo ambalo limemlazimu Mkuu wa Mkoa kutoa maamuzi hayo.
Kaimu afisa ardhi wa halmashauri ya Mji wa Makambako Bi.Flaviana Mambwe amesimama upande wa polisi kusema eneo hilo siyo mali ya wananchi bali ni mali ya polisi huku mkurugenzi wake akisema mpaka wa eneo la polisi ni barabara iliyopo ambayo halmashauri imekuwa ikiilima kwaajili ya wananchi kuitumia jambo ambalo lilimrazimu mkuu wa mkoa kuona kuna ubabaishaji katika kuwatendea haki wananchi na kulazimika kutoa maamuzi ya wananchi kuendelea kujenga na wasibughuziwa na mtu yeyote.

Awali wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopha Ole Sendeka baadhi ya wananchi wa Makambako akiwemo mama mjane aliyekuwa karibu na maeneo ya polisi wamelalamikia idara ya ardhi kutowatendea haki katika kuwalipa fidia za viwanja huku wengine wakinyang'anywa haki zao.

Magreth  William Mkumbo ni mama Mjane anayejishughulisha na biashara ya kuuza uji anasema anamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kusaidia kutatua tatizo lililokuwa likimkabili kwa muda mrefu kwani alikuwa akianza kujenga nyumba yake polisi wanakwenda kumkamata na kumuweka rokapu yeye na mafundi wake ili mradi tu anyanyasike na kuachia eneo hilo ikiwa anazuiliwa yeye tu wenzake waliopo jirani naye wameachwa na kusema kuna kitu gani kinachotendeka na hao polisi.





No comments:

Post a Comment