KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA NJOMBE CHARLES NAKEMBETWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AKIWA OFISINI KWAKE KWAMBA VITENDO VYA RUSHWA VINATAKIWA KUKEMEWA NA KILA MMOJA KIONGOZI NA WANANCHI.
KAIMU MTENDAJI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE EZRA RUBEN KYANDO AKIZUNGUMZA KUHUSIANA NA AMBAVYO WANASHIRIKI KUKABILIANA NA RUSHWA ENEO LA MAHAKAMA KWAMBA WAMEWEKA MABANGO KILA KONA NA WANANCHI WAKIFIKA MAHAKAMANI KUNA NAMBA WAMEWEKA KWAAJILI YA KUTOA TAARIFA KAMA KUNA MTU AMEPOKEA PESA YOYOTE ILI KUPEWA HAKI YAKE.
KAIM MTENDAJI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE AKIZUNGUMZA KWAMBA KWA YEYOTE ATAKAYE ONA AMETOA PESA APIGE SIMU KUPITIA NAMBA ZILIZOPO NJE YA MAHAKAMA HIYO NA NYINGINE AMBAZO ZIPO KWENYE OFISI ZA SERIKALI WAPIGE ILI WAHUSIKA WACHUKULIWE HATUA KALI ZA KISHERIA.
NJOMBE
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU Mkoa wa Njombe imezitaja taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa vinara wa kuendekeza vitendo vya Rushwa Mkoani hapa Ikiwemo jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na mahakama.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Charles Nakembetwa ametaja Taasisi nyingine zilizo lalamikiwa kuhusika na Rushwa kuwa ni Idara ya Afya hususani Hospitali,vituo vya afya Na zahanati,mamlaka za mapato na Halmashauri kuwa na mishahara hewa na watumishi hewa.
Nakembetwa ametumia Fursa hiyo kuwataka viongozi wa serikali wanaosimamia taasisi mbalimbali za serikali na za watu binafsi kuhakikisha zinarekebisha tabia za watumishi wao ili kuacha kuomba rushwa kwa wateja wanaokwenda kupata huduma kwenye ofisi zao.
Aidha kamanda huyo ametaka wananchi kutoa taarifa kwa wakati kabla tukio halijafanyika ili kupata urahisi wa kuwakamata wahusika ambapo hivi karibuni taasisi hiyo inatarajia kuwafikisha mahakamani baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa kuhusika na Rushwa mwaka 2016.
Kaimu Mtendaji wa mahakama Wilaya ya Njombe Ezra Luben Kyando Amesema ili kupunguza malalamiko ya kuhusiana na Rushwa ,Mahakama hiyo imesambaza mabango na namba za simu za bure na za kuripia ambazo wananchi wanatakiwa kupiga pale wanapoona haki haijatendeka.
Baadhi ya wananchi wameshukuru taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Nchini Takukuru Mkoa wa Njombe kwa kuwakamata wahusika na kutaka kuwafikia maeneo yao ya vijijini kutoa elimu ya Kutokomeza Rushwa huku wakisema siri kwa watoa taarifa zinatakiwa kuzingatiwa.
No comments:
Post a Comment