Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, January 11, 2017

MWENYEKITI KITONGOJI IFUNA UTARINGORO AUWAWA


 
 MAREHEMU KASTORY NGAULISA ENZI ZA UHAI WAKE


 WANANCHI WA KIJIJI CHA UTARINGORO WAKITOKA KWENYE ENEO AMBAKO MAREHEMU ALIUWAWA NA WATU WASIYOFAHAMIKA



NJOMBE

Mwenyekiti wa kitongoji cha Ifuna kijiji cha Utaringoro Kastory  Ngaulisa amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiyofahamika akiwa eneo la Msitu wa Udende huku mwenzake akifanikiwa kukimbia baada ya kujeruhiwa mkononi.

Wakizungumza  baadhi ya wananchi na ndugu wa familia ya marehemu wamesema tukio hilo limetokea Januari 6 mwaka huu wakati marehemu huyo na mwenzake Ado Njawike wakitoka shambani kukata nyasi za kurishia ng'ombe.

Wamesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika ambapo majeruhi huyo amelazwa katika hospitali ya Kibena kwa ajili ya matubabu huku wengine wakisema tukio hilo huenda likahusishwa na imani za kishirikina.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Utalingoro  Fadhili Mgaya amelaani kitendo hicho cha mauaji na kutaka wananchi kuonesha ushirikiano kwa jeshi la polisi na viongozi wa serikali ya kijiji katika kuwapata wahusika wa tukio wa hilo.

Diwani wa kata ya Utaringoro Filbert Njawike amesema marehemu baada ya kupata taarifa za tukio hilo wametoa taarifa kwa jeshi la polisi ambapo amepongeza jeshi hilo kwa kuonesha ushirikiano na kutaka wananchi kuwafichua wahusika wa tukio hilo.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Njombe Pudensiana Plotas akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kupokea tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi bado unaendelea wa kuwapata waliohusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment