Wednesday, January 18, 2017
MADIWANI WILAYA WAPEWA SEMINA YA MUUNDO WA KAMATI YA AFYA YA MSINGI KUANZIA NGAZI YA WILAYA,KATA NA VIJIJI
NJOMBE
Halmashauri ya wilaya ya njombe imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa madiwani wa halmashauri hiyo kuhusu muundo wa kamati ya afya ya msingi kuanzia ngazi ya wilaya kata na vijiji.
Akitoa mafunzo hayo kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya njombe Bw michael banyemaa amesema uimarishaji wa huduma za afya ya msingi unalenga katika kuboresha hali ya afya ya jamii kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kuainisha matatizo na mahitaji ya kiafya.
Bwana Manyemaa amesema elimu ya uzazi inatakiwa kutolewa kwa vijana wa kuanzia umri wa miaka 15 hadi 45 ambao wanauwezo wa kushika mimba na kuzaa ili watambue umuhimu wa kujiandaa pindi wanapokuwa wajawazito na kwenda kwenye huduma za afya.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Joram Hongori amesema ni vema madiwani na viongozi wengine wakatambua kuwa kuna umuhimu wa kuwapatia elimu vijana juu ya swala la afya ya msingi kwa walio na umri kuanzia miaka 15 kwani madiwani ni wajumbe wa kamati za afya za kata zao.
Kwa upande wao madiwani wameunga mkono wazo la muwezeshaji kwamba elimu itolewe kwa vijana kuanzia miaka 15 watambua umuhimu wa afya ya msingi ya uzazi ili akina mama wanapokwenda kujifungua katika zahanati na vituo vya afya wawe wamejiandaa kwa kununua mahitaji muhimu yanayohitaji katika uzazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment