SHEKHE WA WILAYA YA NJOMBE MICDAD DINGADINGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA KUAHIRISHWA KWA SHEREHE YA MAURIDI KWA NJOMBE NA KUHUSIANA NA KIKUNDI KINACHOTAKA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU KWENYE MSIKITI HUO
MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI KATIKA MSIKITI MKUU WA NJOMBE MJINI JUMA LUKUVI
JUMA LUKUVI MWENYEKI WA ULINZI MSIKITI MKUU WA NJOMBE MJINI
NJOMBE
Wakati waumini wa dini ya kiislamu wakiadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamed Nchini Kote,Waumini wa dini hiyo wameingiwa na hofu ya kutokea kwa uvunjifu wa amani katika msikiti Mkuu wa Njombe Mjini kutokana na kudaiwa kuwepo kwa kundi la watu wanaotaka kuharibu amani iliyopo msikitini hapo.
Kauli hiyo imetolewa na Shekhe Wa Wilaya Micdadi Dingadinga wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kuhusiana na Njombe kuahirisha sherehe ya kuzaliwa kwa mtume Muhamad ambayo waumini wa Wilaya ya Njombe wataadhimisha Decemba 24 mwaka huu na kusema kuwa kumeibuka kikundi kinachotaka kuharibu amani ya waumini wa msikiti huo.
Shekhe Dingadinga amesema viongozi wa msikiti Mkuu wa Njombe Mjini tayari wamejiandaa kukabiliana na tatizo lililopo kwenye msikiti huo kwani wametoa taarifa kwa vyombo vya dola kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Msikiti Mkuu wa Njombe Mjini ili kuimarisha amani ya waumini wa dini hiyo.
Kuhusu sherehe ya Maurid Shekhe Dingadinga amesema waumini wa dini hiyo wanaadhimisha sherehe hiyo kwaajili ya kukumbuka historia ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad ambaye katika itikadi za uislamu ni mtume wa mwanzo pia ni mtume wa mwisho ambaye amezaliwa siku ya jumapili kuamkia jumatatu katika Nchi ya Maka aliyeizungumza kwa ufasaha zaidi dini ya kiislamu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa Msikiti mkuu wa Njombe Mjini Musa Lukuvi amewatoa hofu waumini wa dini ya Kiislamu katika msikiti huo kwamba kikundi kinachotaka kuvuruga amani kitakwenda kuchukuliwa hatua za kisheria pindi kitakapojaribu kufanya tukio la uharifu ambapo usalama umeimarishwa kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Sherehe Ya Maurid Kitaifa hapo jana imefanyika katika Mkoa wa Singida Mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa ambapo kwa Wilaya ya Njombe imeahirishwa hadi tarehe 24 mwezi huu itakapoadhimishwa kwani sherehe hiyo inakwenda hadi decemba 29 kwaajili ya waumini wa dini hiyo kukumbuka Historia ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad .
No comments:
Post a Comment