Matroni
wa Kituo cha Afya cha Murangi, Sabina Daudi akitoa shukrani kwa Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) baada ya
kupokea vifaa kwa ajili ya kituo hicho.
Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa. Wa kwanza
kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Thadeus Makwanda
na katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murangi,
Dkt. Josephat Karambo.
Mbunge
wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (kushoto) akiwasili katika Kituo cha Afya cha Murangi
kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Musoma, Dkt. Vicent Naane.
Baadhi ya Vitanda ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa katika Kituo cha Afya cha Murangi.
Mbunge
wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo amesikitishwa na wizi wa dawa na uharibifu wa baadhi ya vifaa
katika Kituo cha Afya cha Murangi, Musoma Vijijini na kuagiza wahusika
wachukuliwe hatua.
Agizo
hilo alilitoa hivi karibuni wakati akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali
vya afya ikiwemo vitanda maalum 10, baisikeli za wagonjwa na vifaa
vingine kutoka kwa wafadhili wa Australia kwa ajili ya Kituo hicho na
kushuhudiwa na wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya jimbo hilo.
Awali
kabla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, alipokea taarifa kutoka kwa
wananchi kuhusiana na wizi wa dawa uliomhusisha mlinzi wa Kituo hicho
pamoja na tukio la kuharibiwa kwa gari la wagonjwa alilokabidhi mwezi
Machi mwaka huu.
Taarifa
husika ilimkasirisha Profesa Muhongo na hivyo kuagiza wahusika wote
wachukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekanavyo ili iwe fundisho kwa
wenye tabia za namna hiyo.Akizungumzia gari hilo, Profesa Muhongo
alisema lilitolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya wananchi wa jimbo
la Musoma Vijijini lengo likiwa ni kusaidia wananchi hao kuondokana na
usumbufu waliokuwa wakiupata.
Aliongeza
kuwa Serikali hiyo ya Japan ilimuahidi magari mengine zaidi ikiwa gari
hilo litatunzwa vizuri na kutumika kwa shughuli iliyokusudiwa.“Hii ni
aibu kubwa, hata wafadhili watatushangaa na kutucheka, dawa nyingi
tulipewa na wafadhili na gari ile tulikabidhiwa ikiwa bado mpya na kwa
Tanzania gari za namna hiyo zipo mbili tu, ni hapa na Muhimbili,”
alisema.
Mbali
na hilo aliongeza kuwa Serikali ya Japan ilitoa kiasi cha shilingi
milioni 170 kwa ajili ya kuboresha Kituo hicho na kuongeza kuwa
atamuomba Balozi wa Japan nchini kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha
hiyo.Aliwaagiza Madiwani kufuatilia kubaini hatua iliyofikiwa ya
matumizi ya fedha hiyo na alisema endapo itadhihirika kuna ubadhirifu wa
aina yoyote hatua za kisheria zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kurejesha
fedha hizo.
Profesa
Muhongo alisema anashangazwa kupewa taarifa hiyo na wananchi huku
viongozi wakiwa kimya bila kuonesha hatua walizochukua na hivyo
aliwataka Madiwani kutokuwa waoga katika kuwachukulia hatua wanaofanya
ubadhirifu.Aidha, Profesa Muhongo aliwaagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Musoma, Dkt. Thadeus Makwanda na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha
Afya cha Murangi, Dkt. Josephat Karambo kuhakikisha hadi kufikia Tarehe
15 mwezi ujao gari hilo liwe limetengemaa.
No comments:
Post a Comment