MJIENDELEZE MSIISHIE HAPO MLIPOFIKIA-MWAKYEMBE.
Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amewataka wahitimu wa astashada na stashada za
Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kujiendeleza zaidi kielimu ili
waweze kwenda na wakati hasa ikizingatiwa kuwa dunia ya sasa inataka
kujiendeleza kila siku vinginevyo wataachwa nyuma.
Mhe. DKT Mwakyembe ametoa rai
hiyo alipowatunuku vyeti vya Astashahada na Stashahada wahitimu hao katika
ukumbi wa Jaji Nyalali uliopo chuoni hapo mjini Lushoto.Amewataka wahitimu hao kuwa
tayari kulihudumia taifa kwa kufanya kazi kwa moyo na kuepuka kujihusisha na
vitendo vya rushwa kwa kuwa rushwa ni adui mkubwa wa haki duniani Amewataka wahitimu hao kuwa
tayari kuwahudumia wananchi katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kuwa serikali
iko mbioni kutunga sheria ya ahuduma ya msaada wa kisheria ambayo itawawezesha
wananchi wenye uhitaji kupata huduma za kisheria kupitia wasaidizi wa kisheria.
"Niwaambie ninyi
mliohitimu hapa leo mna bahati sana, Serikali sasa inatunga Sheria ya Msaada wa
huduma za kisheria , umeshasomwa Bungeni kwa mara ya kwanza na Bunge likiupitisha
na kuwa Sheria mtaweza kufanya kazi kama wasaidizi wa sheria na hivyo
kuwahudumia wananchi wengi wenye uhitaji na kusaidia harakati za utoaji haki
nchini," alisema Dkt Mwakyembe.Amesema kutungwa kwa sheria
hiyo kutawawezesha wahitimu hao kuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa
kuwapa msaada wa kisheria wananchi hasa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama
za mawakili.
Dkt Mwakyembe ametunuku vyeti
vya astashahada kwa wahitimu 135 na stashahada kwa wahitimu 208 katika Mahafali
ya 16 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Lushoto mkoani Tanga.
Wakati huo huo Chuo hicho cha
IJA kimezindua NEMBO yake , Tovuti mpya ya Chuo na mfumo wa mawasiliano kwa
barua pepe kutumia mtandao wa Serikali.Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa vitu hivyo Mkuu wa Chuo hicho Mhe. Jaji Dkt Paul Kihwelo
alisema sio kwamba Chuo hakikuwa na
Nembo na Tovuti ila yanefanyika marekebisho makubwa katika vitu hivyo ili
kwenda na wakati.
Alisema kwamba Chuo ndio kimeanza kutumia barua pepe kwa kutumia mtandao wa
Serikali ambapo kwa sasa utawahusu watumishi wa chuo hicho kama ilivyo kwa
taasisi nyingine za Serikali na wanatarajia pia kuwaunganisha wanafunzi hapo
baadae.
No comments:
Post a Comment