Na Zainab Nyamka,
BENKI
ya DCB yaibuka kidedea kwa kupata zawadi ya kwanza kwa sekta ya benki
ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu
kwa mwaka 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa
DCB Edmund Mkwawa amesema kuwa hii ni tuzo inayoandaliwa kila mwaka na
bvodi ya uhasibu Tanzania (NBAA) ambapo yalianza toka mwaka 2011.
Mkwawa
amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne benki ya DCB imeweza
kufanya vizuri kwa kushika nafasi tatu za juu na kuwa moja ya miongoni
mwa benki zinazofanya vizuri na katika uandaaji na uwasilishaji wa
taarifa za hesabu na kwa mwaka 2015 imeweza kushika namba moja.
Amesema
kuwa benki yao inafuata miongozo ya utawala bora na kuwataka wawekezaji
kuwa na imani juu ya usalama wa fedha zao walizoziwekeza na kuahidi
kuendeleza mafanikio hayo kiujumla.
Mkwawa
ameweka wazi mafanikio ya benki hiyoikiwemo ni kutimiza miaka 14 ya
utoaji huduma bora za kibenki kwa wajasiliamali, kuongezeka kwa matawi
kutoka mawili mwaka 2005 hadi matawi tisa 2016 na mwakani 2017
wanatarajia kufungua tawi la 10 mkoani Dodoma.
Mafanikio
hayo ni pamoja na kuwa na mtaji imara wa bilioni 32 na upanuaji na
uboreshaji wa huduma za kisasa kwa wateja wetu kupitia mawakal ambapo
watawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia mawakala
walioidhinishwa na DCB katika vitongoji kwa kupitia DCB PESA
inayotarajiwa kuanza Januri 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari juu ya zawadi waliyoipata kwenye sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akiwa ambebebelea zawadi waliyoipata ya sekta
ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa
za hesabu kwa mwaka 2015, pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akionyesha kifaa kitakachokuwa kinatumiwa
na mawakala wa benki hiyo katika mfumo utakaoenda wa DCB PESA
unaotarajiwa kuanza Januari 2017.
Mawakala wa DCB wakiwa makini kusikiliza.
No comments:
Post a Comment