Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akieleza jambo kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika
ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa(kushoto) ambaye yupo nchini kwa ziara ya
kikazi kwa siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya nchi
hizo kupitia Sanaa na Utamaduni ikiwemo kuhifadhi historia ya ukombozi
wa Afrika ya Kusini leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole
Gabriel (kulia) akisalimiana na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika
ya Kusini Ndg.Nathi Mthehwa (Kushoto) leo Jijini Dar es Salaam
alipotembelea Wizara hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano
baina ya nchi hizo katika sekta za Sanaa na Utamaduni, katikati ni
Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Thamsanga Dennis Mseleku.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akiongea
na waandishi wa habari (hawapo katika Picha) leo Jijini Dar es Salaam
kuhusu ziara ya Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg.
Nathi Mthehwa ambaye
yupo nchini kwa siku tatu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya
nchi hizo kupitia sekta ya Sanaa na Utamaduni ikiwemo kuhifadhi historia
ya ukombozi wa Afrika ya Kusini.
Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika
ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa (kulia) akizungumza katika mkutano wa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara yake ya siku tatu
nchini leo Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye .
Mshauri Mtaalamu wa Urithi wa Utamaduni Dkt.Daniel Ndagala akichangia hoja wakati wa kikao baina ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa leo Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe
kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini wakifuatilia kwa makini mazungumzo
baina ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses
Nnauye na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa katika mkutano wao na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (wanne
kushoto)na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg.Nathi
Mthehwa(wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini baada ya kumaliza kwa kikao leo
Jijini Dar es Salaam.Picha Na Lorietha Laurence – WHSUM
Na Genofeva Matemu - WHSUM.
Serikali
ya Tanzania itaendelea kuweka historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika
kwa kuhifadhi kumbukumbu zote huku ikitunza na kuweka alama maeneo
ambayo yalitumika wakati wa kupigania Uhuru wa Bara la Afrika na kutunza
makaburi ya wapigania uhuru hao pamoja na kuyafanya kuwa ya kihistoria.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Waziri wa
Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe.Nathi Mthehwa aliyeko nchini
kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi hizo
mbili katika sekta ya Utamaduni na Sanaa.
“Tumeanza
kuandika historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika kwa kuhoji baadhi ya
wanaharakati walioshiriki katika kuwasaidia wapigania uhuru kuanzisha
vyama vyao vya ukombozi ambapo historia hii itahifadhiwa kwa njia ya
sauti na picha lakini pia tutaendelea kutunza kumbukumbu zote
tutakazozipata na kuwekea alama maeneo ambayo yalitumika wakati wa
kupigania uhuru” amesema Mhe. Nnauye
Aidha,
Mhe. Nnauye amesema kuwa makubaliano yaliyosainiwa mwaka 2011 kati ya
Tanzania na Afrika ya Kusini kufuta Visa ya kusafiria kati ya nchi hizo
mbili yameleta mabadiliko makubwa katika eneo la Sanaa nchini kwani
wasanii wamekua wakitumia fursa hiyo kwenda Afrika ya Kusini kuandaa
kazi zao na kuzifanya kuwa na ubora zaidi.
Kwa
upande wake Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika Kusini Mhe. Nathi
Mthehwa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano
uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuthamini mchango uliofanywa na
Tanzania katika kukomboa nchi ya Afrika ya Kusini.
Pamoja
na hayo Mhe. Mthethwa ameahidi kuendeleza ushirikiano ulipo na
kuthamini maendeleo yaliyopo kwenye maeneo ya Utamaduni na Sanaa kwa
kuhakikisha kuwa mafanikio ya Sekta za Ubunifu ndani ya Afrika ya Kusini
yanakua sehemu ya mafanikio ndani ya nchi ya Tanzania.
Ziara
hii inaangalia namna nchi hizi mbili zinaweza kuimarisha makubaliano ya
mwaka 2011, katika maeneo mengine ya mashirikiano kama vile upande wa
tasnia ya filamu ambapo Afrika ya Kusini imekua ikifanya vizuri ikiwemo
kusimamia haki za wasanii kwa kutengeneza mifumo ya kisheria ya kulinda
haki za ubunifu na kuongeza mahusiano ya nchi hizo mbili.
Waziri
huyo atatembelea Mkoa wa Morogoro kwenye kambi ya wapigania Uhuru wa
Afrika ya Kusini Mazimbu, Dakawa pamoja na Bagamoyo ambapo kulikua na
kambi yao,pamoja na baadhi ya maeneo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment