Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, October 27, 2016

WANANCHI IDETE WATARAJIA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA ZA AFYA BAADA YA KANISA KATHOLIKI JIMBO LA NJOMBE KWENDA KUANZA UJENZI WA ZAHANATI

NJOMBE

Wananchi wa kitongoji cha Idete kata ya Mfriga Wilayani Njombe Wametakiwa kuonesha ushirikiano katika ujenzi wa zahanati inayojengwa na kanisa katholiki jimbo la Njombe ili kupata huduma za afya karibu nao Tofauti na awali.

Rai Hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Lupembe Joram Hongori wakati akizungumza na wananchi hao kwenye kitongoji kilichopo umbali wa kilomita 20 kutoka makao makuu ya Kijiji cha Itambo ambacho huduma za afya na Elimu ni changamoto kubwa kwao.

Mbunge Hongori amemshukuru Muhashamu Askofu Alfred Maluma wa jimbo la Njombe na waumini wake kwa kuanza kusogeza huduma za Afya na Elimu kwa wananchi wa kitongoji hicho ambapo amesema halmashauri ya Wilaya ya Njombe inatakiwa Kuunga mkono  juhudi za kanisa hilo za kusogeza huduma muhimu kwa jamii.

Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi wa shule na zahanati Idete  Muhasibu wa jimbo katholiki Njombe Padre Camillo Mdeya amesema kanisa hilo limelazimika kuanzisha shughuli za ujenzi wa shule na zahanati baada ya kuona wananchi wa kitongoji cha Idete wanapata tabu ya kufuata huduma muhimu za afya na elimu.

Padre Mdeya Amesema wamependekeza kuwa zahanati itaitwa Chiantole Dispensary na shule itaitwa Colombo Primary school kutokana na mapadre walioanza kufika kwenye kijiji hicho kwa nia ya kutoa huduma kwa wakazi wa kitongoji hicho ambapo ujenzi wa zahanati Unatarajia kukamilika ifikapo mwezi decemba mwaka huu.


 Wananchi na mwenyekiti wa kitongoji cha Idete Leoty Mgute wamesema kilio kikubwa ambacho kimekuwa kikiwakumba na kubeba wagonjwa na wajawazito kwa kutumia machela hadi zahanati ya Itambo au kituo cha afya Lupembe ambapo kujengwa kwa zahanati ni ukombozi mkubwa kwao.

No comments:

Post a Comment