Katibu wa mbunge jimbo la Isimani Bw Thom Malenga kulia akimkabidhi diwani wa Mboliboli Khalfan Lulimi msaada wa bati kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katani kwake msaada huo umetolewa na mbunge Wiliam Lukuvi kwa kata mbali mbali kwa kutoa bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 na Power tila 15 kwa madiwani wote wa CCM jimboni mwake .
Diwani wa Mlolo Charles Nyagawa kushoto akikabidhiwa bati na katibu wa mbunge wa Isimani Thom Malenga .
Madiwani wakipokea bati
Diwani wa viti maalum Idodi Sophin Msekwa akipokea msaada wa badi
Diwani wa Mlenga akipokea bati
Diwani wa kata ya Malenga makali Flanzisca Kalinga akiwa akijiandaa kuendesha moja kati ya Power tila 15 zenye thamani ya Tsh milioni 105 zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa Wiliam Lukuvi kwa ajili ya madiwani wote 15 wa CCM jimboni mwake kama miradi yao pamoja na bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo jimboni humu wa tatu kushoto ni katibu wa mbunge Lukuvi , Thom Malenga ambae alikabidhi kwa niaba ya mbunge Lukuvi akiwa na baadhi ya madiwani hao
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi aametoa msaada wa bati 2000 ajili ya kukamilisha miradi ya kimaendeleo katika kata mbali mbali za jimbo hilo pamoja na kuwasaidia madiwani wote 15 wa chama cha mapinduzi (CCM) Power Tila vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 100.44
Lukuvi alisema amelazimika kukabidhi msaada huo wa power tila kwa madiwani wake ili kuwawezesha kiuchumi pia kusaidia kusukuma maendeleo katika kata zao kama kuwasaidia wananchi kutumia power tila hizo kuendeshea shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo za kilimo.
Kwani alisema kuwa power Tila hizo amezinunua zikiwa na kamili ya vifaa vyake vyote kama jembe la kulimia pamoja na tela zake kwa ajili ya kusafirishia mazao ama kufanyia shughuli nyingine za kijamii katika kata .
Akikabidhi msaada huo leo kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wake Thom Malenga alisema kuwa kuwa lengo la msaada huo ni kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa jimbo la Isimani na kuwa msaada wa bati unakwenda katika kata zote ambazo zina miradi ya ujenzi wa shule ,nyumba za walimu na zahanati ambazo zilikuwa zikihitaji bati ili kumalizia ujenzi huo na kuwa bati zote ziliotolewa ni 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44
Wakati msaada huo wa power Tila umeelekezwa kwa madiwani 15 wa CCM waliopo katika jimbo hilo na kuwa kila power tila moja imegharimu kiasi cha Tsh milioni 7 na kwa powertila zote zimegharimu Tsh milioni 105 lengo kubwa la kutoa msaada huo ni kuwawezesha madiwani hao kuwa na vitega uchumi na kuongeza ari ya kuwatumikia wananchi wao .
Hivyo alisema kuwa kupitia msaada huo wa bati anaamini madiwani hao wakiwa ni wenyeviti wa kamati za maendeleo ya kata kuhakikisha wanasimamia vema miradi ya ujenzi inayoendelea katika maeneo yao na kwa upande wake mbunge ameamua kutoa msaada huo wa bati kama njia ya kuwapunguzia makali wananchi wake kwa ajili ya kuchangia pesa kununua bati hizo.
" Mheshimiwa mbunge amewaunga mkono wananchi kwa kazi waliyoifanya ya kusimamisha kuta za vyumba vya madarasa na zahanati na kwa ajili ya kuwaunga mkono bati amelazimika kununua "
Hata hivyo alisema kwa upande wa power Tila hizo alisema ni mradi binafsi wa madiwani wake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wao hivyo kazi ya diwani na kusimamia shughuli za kimaendeleo na pale wananchi wanapohitaji msaada wa power tila hizo basi mwenye mamlaka nazo ni diwani mwenyewe na sio mradi wa kata wala kijiji .
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa na diwani wa kata ya Mboliboli Khlfani Lulimi akishukuru kwa niaba ya madiwani wenzake alisema kuwa msaada huo ni mkubwa kwao na zaidi wanampongeza mbunge wao kwa kuthamini kazi inayofanywa na madiwani na kuwa watahakikisha power tila hizo zinaleta chachu ya maendeleo katika maeneo yao.
Wakati diwani wa kata ya Malenga Makali FLanzisca Kalinga na diwani wa viti maalum tarafa ya Idodi Sophin Msekwa pamoja na kupongeza msaada huo walisema wanategemea kutumia power tila hizo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na watoto hasa ukizingatia kuwa kumwezesha mwanamke ni kuisaidia jamii nzima.
No comments:
Post a Comment