DIWANI KATA YA RAMADHANI AKIWA MGENI RASMI HAPA ANASALIMIANA NA MKURUGENZI WA SHULE HIYO BI. ANNA Zocca PAMOJA NA WALIMU WENGINE WA SHULE HIYO
Wanafunzi wanaobaki wakiburudisha umati wa wazazi waliofika kusherehekea sherehe hizo
Hawa ni wazazi wakitoa nasaha kwa wanafunzi wanaobaki na wanaoondoka na kwa wazazi wengine wenye tabia za kutowaendeleza masomo
WANAFUNZI WA SEKONDARI NAO HAWAKUWA NYUME WAKASOMA RISALA KWA MGENI RASMI
NJOMBE
Diwani wa kata ya Ramadhani
mjini Njombe Menson Geoge Sanga ameahidi kuzitatua changamoto za ukosefu
wa huduma za maji katika taasisi
mbalimbali za elimu na
afya kwa kushirikiana na mamlaka ya maji Njombe mjini JUWASA.
Diwani wa kata ya Ramadhani
bwana Sanga ametoa Ahadi hiyo wakati
akiwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya 13 ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Mtakatifu
ST.Benedict.
Bwana Sanga amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa maji ya bomba kwa
baadhi ya mitaa ya kata hiyo serikali imeliona tatizo na kuanza kutekeleza kwa
baadhi ya mitaa ikiwemo mitaa ya Kibena.
Akimkaribisha Mgeni rasmi
kuzungumza na wazazi na wanafunzi wanaoagwa na wanaobaki mkurugenzi wa shule ya
St.Benedict Anna Zocca Amepongeza wazazi kwa ushirikiano walioonesha
na kutaka waendelee nao ili kutoa elimu bora kwa watoto.
Awali akisoma risala fupi kwa
niaba ya wanafunzi wanaoagwa Tunukiwa
Magwaza amesema jumla ya wanafunzi 47 wa
darasa la saba wanakwenda kufanya mtihani wa mwisho wa Taifa unaotarajia kuanza
wiki ijayo na kwamba shule hiyo
inakabiliwa na tatizo la kukosekana kwa huduma za maji na kukwamisha jitihada
za masomo.
Kwa Upande Wao baadhi ya
wazazi wakizungumza mbele ya mgeni rasmi wameshukuru uongozi wa shule hiyo kwa
kuwalelea watoto wao vizuri kimaadili,na kidini
huku wakiomba wanafunzi hao kwenda kuendelezwa kimasomo
pindi watakapo kuwa wamefauru mtihani wa taifa.
No comments:
Post a Comment