HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA IDINDILIMUNYO WILAYANI WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE WAKIWA KWENYE MAANDAMANO YA KUELEKEA KWA MKURUGENZI WA WILAYA HIYO.
DIWANI WA KATA YA IGWACHANYA ANTONY MAHWATA AKIWA KWENYE KIKAO CHA DHARULA CHA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA WILAYA YA WANGING'OMBE AKIWA NA KWENYE MAWAZO JUU YA KUANDAMANA KWA WANANCHI HAO KWENYE KATA YAKE.
AFISA ELIMU SHULE ZA MSINGI WILAYA YA WANGING'OMBE MWALIMU HARUNA SEREMANI AKITOA TAARIFA YA SHULE ZENYE WALIMU WACHACHE ZAIDI KULIKO SHULE HIYO KWAMBA KUNA SHULE WILAYA YA WANGING'OMBE ZINAWALIMU WATATU.
HUYU NI MWENYEKITI WA KIJIJI CHA IDINDILIMUNYO GODEN KASANGA AKIZUNGUMZA JUU YA KILE KILICHOWAPELEKA KWA MKURUGENZI WA WILAYA HIYO.
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ALLY KASINGE AMBAYE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA HIYO.
MKURUGENZI WILAYA YA WANGING'OMBE AMINA KIWANUKA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA IDINDILIMUNYO BAADA YA KUWASILI KWENYE UKUMBI WA KIKAO HICHO CHA DHARULA.
HAPA WANANCHI WANATOKA KUELEKEA MAKWAO BAADA YA KUPOKEA USHAURI KUTOKA KWA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA
HAPA NI SAFARI BILA MAANDAMANO INAANZA YA KUELEKEA NYUMBANI KWAO IDINDILIMUNYO
Wananchi Wa Kijiji Cha Idindilimunyo Kata Ya Igwachanya Wilayani Wanging'ombe Leo Wamefanya Maandamano Ya Amani Yasiyo Zingatia Taratibu Za Kisheria Hadi Kwa Mkurugenzi Ili Kushinikiza Halmashauri Hiyo Isimuhamishe Mwalimu Wa Shule Ya Msingi Idindilimunyo Kwenda Shule Ya Msingi Lyamluki Kwa Kile Walichodai Kuwepo Kwa Upungufu Wa Walimu.
Wakizungumza Na Uplands Fm Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Idindilimunyo Wilayani Wanging'ombe Wamesema Wanashindwa Kufahamu Sababu Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Hiyo Kumuhamisha Mwalimu Huyo Pasipo Kuwapelekea Mwalimu Mwingine Wa Kuziba Nafasi Ya Anayehama Ikiwa Bado Wanauhitaji Wa Walimu Watatu Kuziba Myanya Ya Walimu Waliostaafu Mwakajana.
Aidha Wananchi Hao Wakiongozana Na Mwenyekiti Goden Kasanga Wamelaumu Uongozi Wa Kata Ya Igwachanya Kuwa Huenda Umefanya Njama Za Kumuhamisha Mwalimu Huyo Kupitia Mwenyekiti Wa Halmashauri Ambaye Ni Diwani Wa Kata Hiyo Kutokana Na Wananchi Hao Kugomea Kuchangia Fedha Za Madawati Kwa Kile Walichodai Wanajenga Vyoo Kwanza Ndipo Madawati Yafuate Mwakani.
Akizungumza Kwenye Kikao Cha Dharula Mwenyekiti Wa Kamati Ya Ulinzi Na Usalaama Ambaye Ni Mkuu Wa Wilaya Ya Wanging'ombe Muhamed Ally Kasinge Amewaonya Wananchi Hao Kwamba Wamekiuka Kanuni Na Sheria Zilizowekwa Za Kufanya Maandamano Kwani Wanaweza Sababisha Matatizo Makubwa Nakwamba Walipaswa Kujadili Kama Ajenda Na Kuziwasilisha Ofisi Ya Kata Ili Waweze Kusikilizwa .
Kasinge Amesema Kuwepo Na Walimu Saba Hakuwezi Kuathiri Masomo Shuleni Na Kwamba Kuna Shule Nyingine Wilayani Humo Zina Walimu Chache Kabisa Kuwanzia Watatu, Wanne Huku Afisa Elimu Wilaya Ya Wanging'ombe Haruna Seremani Akisema Mwalimu Ambaye Wananchi Wanashinikiza Asihamishwe Amepangiwa Shule Ya Msingi Lyamluki.
Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Wanging'ombe Amina Kiwanuka Amewataka Wananchi Kuyaweka Kwenye Maandishi Mawazo Yao Ya Kuhitaji Walimu Ili Halmashauri Iweze Kuyashughulikia Huku Akisema Maandamano Yao Yamekiuka Sheria Na Kanuni Na Kusema Viongozi Wanatakiwa Kufanya Majadiliano Kabla Ya Kufanya Maandamano .
....................................................................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment