HILI NI ENEO LA MAKABURI YA KIBENA ALIPOZIKWA MAREHEMU HASSAN HABIBU JUMA
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE ANTONY MAHWATA MWENYE SUTI NYEUSI KULIA NA ALIYEVAA MIWANI MKONO WA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ALLY KASSINGE WAKIWA PAMOJA NA WANANCHI KWENYE MAZISHI YA MTUMISHI WAO.
UMATI WA WANANCHI WA NJOMBE MJINI NA WILAYA YA WANGING'OMBE WAKIWA MAKABURINI
MWENYE BARAGASHIA NI IMAMU WA MSIKITI MKUU WA NJOMBE MJINI RAJAB MSIGWA AKIONGEA NA UMATI MAKABURINI HAPO
MUWAKILISHI WA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE JUMA CHALAMILA AMBAYE NI AFISA UTUMISHI WILAYA
NI BAADA YA MAZISHI SASA WANANCHI NA VIONGOZI MBALIMBALI WANARUDI NYUMBANI KWA MAREHEMU BAADA YA ZOEZI LA MAZISHI KUKAMILIKA
Wananchi Mkoani Njombe Wametakiwa kuwasaidia watu wasiyo jiweza kwa kutoa misaada mbalimbali na kujenga tabia ya kuwatembelea wagonjwa na kuacha tabia ya kutumia uwezo wao wa mali walizonazo kuwanyanyasa wasiyojiweza waliopo karibu nao .
Rai hiyo imetolewa na Imamu wa msikiti Mkuu wa Njombe mjini Rajab Msigwa wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Hassan Habibu Juma ambaye amefariki Augost 27 akiwa nyumbani kwake Nazareth.
Imamu Msigwa ametumia fursa hiyo kuwaomba wenye uwezo wa mali kusaidia makundi ya wasiyojiweza na wajane huku wakiimarisha swala tano wakati wa uhai wao ili wasiulizwe na mwenyezi Mungu juu ya Neema ya mali walizokuwa nazo ambapo ameomba waumini kusamehe waliowakosea na wao watasamehewa na Mungu.
Akisoma Historia ya marehemu Hassan Habibu Juma kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe ,Afisa utumishi Juma Chalamila amesema marehemu alifariki ghafra kwa ugonjwa wa presha akiwa nyumbani kwake baada ya kutoka Mkoani Mbeya alikokwenda kikakazi kabla ya kufariki.
Akizungumza na waandishi mara baada ya mazishi ya marehemu Hassan Habibu Juma mwenyekiti wa Umoja wa madereva wa halmashuri Mkoa wa Njombe Patrick Mfikwa amesema kifo cha mwanachama mwenzao kimeacha pengo kubwa kwa serikali na kwa umoja huo.
No comments:
Post a Comment