Monday, July 4, 2016
WATATU WAFARIKI PAPO HAPO KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI LEO NJOMBE
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE PUDENSIANA PLOTAS AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE.
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Vifo Vya Watu Watatu Vilivyotokana Na Matukio Mawili Ya Ajali Za Pikipiki Kugongwa Na Magari Likiwemo La Mwendesha Pikipiki Waiton Wilfred Mwenye Umri Wa Miaka 32 Mkazi Wa Lyamkena Mjini Makambako Ambayo Imetokea Eneo La Lutilage Barabara Ya Njombe Songea Iliyotokea Majira Ya Saa Kumi Na Moja Alfajiri.
Akizungumza Na Uplands Fm Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Pudensiana Plotas Amesema Gari Ambalo Halikufahamika Namba Wala Dereva Wake Likiwa Linatokea Mjimwema Kuelekea Makambako Limemgonga Dereva Wa Pikipiki Namba T 411 BQG Aina Ya Sunlg Iliyokuwa Ikiendeshwa Na Waiton Wilfred Na Kumsababishia Kifo Chake Huku Dereva Akikimbilia Kusikojulikana.
Kamanda Plotas Amesema Jeshi La Polisi Linaendelea Na Jitihada Za Kutafuta Gari Hilo Na Dereva Wake Huku Wananchi Wakiombwa Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Hilo Katika Kufanikisha Kulipata Gari Na Dereva Aliyekimbia Ili Aweze Kufikishswa Kwenye Vyombo Vya Sheria Kujibu Tuhuma Zinazomkabili Ambapo Chanzo Cha Ajali Hiyo Bado Kinachunguzwa .
Katika Tukio Lingine Watu Wawili Wamefariki Baada Ya Pikipiki Waliyokuwa Wakitembelea Kugonga Gari Aina Ya Canter Na Kusababisha Kifo Cha Yustin Kihombo Na Damas Lulambo Ambaye Alikuwa Dereva Wa Pikipiki Hiyo Aina Ya Boxer Tukio Ambalo Limetokea Majira Ya Saa Tatu Asubuhi Ambapo Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.
Kamanda Plotas Ametoa Wito Kwa Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kuwa Makini Na Kufuata Taratibu Za Sheria Za Usalama Wa Barabarani Huku Akisema Ajali Ikitokea Madereva Wanapaswa Kujisalimisha Kwenye Kituo Cha Polisi Kwa Usalaama Wao Kuliko Kutoroka Mara Wanapokuwa Wamesababisha Ajali Hizo.
Kwa Upande Wake Afisa Mtendaji Wa Kijiji Cha Kichiwa Erasto Kapinga Amesema Gari Hilo Aina Ya Canter Lilikuwa Likivuka Barabara Kuelekea Upande Wa Pili Lakini Dereva Wa Pikipiki Alishindwa Kutambua Mapema Na Kusababisha Pikipiki Kujigonga Kwenye Gari Hilo Na Kutokea Vifo Hivyo Vya Papo Hapo Vya Wakazi Wa Kijiji Cha Kichiwa.
Awali Wakizungumza Na Uplands Fm Baadhi Ya Mashuhuda Wa Tukio Hilo Wamesema Mwili Wa Marehemu Umekutwa Kwenye Mtaro Wa Maji Majira Ya Saa Kumi Na Moja Alfajili Ukiwa Hauna Kichwa Ambapo Majira Ya Saa Moja Asubuhi Kichwa Kimeonekana Umbali Wa Takribani Mita 30 Kutoka Eneo La Ajali Huku Ubongo Ukionekana Kuachana Na Kichwa Hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment