Mtoto Clara Damian mwanafunzi wa darasa la saba asiyeona akiwa darasani akitumia mashine maalumu ya kuandikia na kusoma katika shule ya msingi patandi iliyopo wilaya ya arumeru mkoani arusha shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu na vitabu.
Na Woinde Shizza,Arusha.
Wanafunzi
wenye ulemavu katika shule ya msingi Patandi iliyopo wilaya ya Arumeru
Mkoani Arusha wamelalamikia tatizo la upungufu wa walimu,vitabu na vifaa
vya kufundishia kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu hali
inayokwamisha maendeleo ya kitaaluma hivyo wameiomba serikali na taasisi
binafsi kutatua changamoto hiyo.
Mwanafunzi
asiyeona anayesoma darasa la saba Clara Damian ni alisema kuwa kumekua
na uhaba wa vitabu kwa watoto wasioona na mashine za kuandikia maandishi
yenye nundu ambazo ni chache na kwa sasa ni mashine tatu pekee
zinafanya kazi ukilinganisha na idadi kubwa ya wanafunzi.
Alisema
kuwa miundombinu ya majengo ya madarasa pia yamekua si rafiki kwa
watoto wenye ulemavu hivyo anashauri miundombinu ya majengo na shule
iendane na mahitaji wa watoto hao.
Mibaku Limba Mwanafunzi asiyesikia (kiziwi) alisema kuwa
walimu walioko kwa sasa wanaofundishwa kwa lugha za alama ni
wachache ukilinganisha na idadi ya masomo hali ambayo inachangia
kuwarudisha nyuma.
Mratibu wa Kitengo Cha Walemavu Mwalimu Anna Shayo Katika Shule
hiyo Mwalimu Shayo alikiri kuwepo kwa upungufu wa walimu na vitabu
kwa watoto wenye mahitaji maalumu na kuiomba jamii,taasisi na
serikali kushiriki katika kuboresha maendeleo ya watoto hao ambao
wakijengewa misingi bora ya elimu wanaweza kuwa na mchango kwa jamii
badala ya kuwa tegemezi.
Mwalimu
Marko Alois Mamuya anayefundisha watoto viziwi ameiomba serikali itoe
motisha kwa walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalumu ili
kuongeza ari na hamasa itakayosaidia kupata idadi kubwa ya walimu.
“Tunawaomba
wazazi wasiwafiche watoto wenye ulemavu majumbani bali wawalete
mashuleni huku waweze kupata elimu ,lishe na mazoezi badala ya
kuwafungia nyumbani kwani wanazidi kuwa tatizo licha nya uwezo,vipaji na
ubunifu walioanao ambao unaweza kuwasaidia wao na jamii yao” alisema
Mwalimu Marko.
No comments:
Post a Comment