Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa mashujaa waliojitoa
kwa uzalendo kupigania Tanzania hawana budi kukumbukwa kutokana na
kujitoa kwao ili Tanzania isitawaliwe na wakoloni.
Makonda
ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa katika Mkoa
wa Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam, amesema kuwa mashujaa hao walifanya ukombozi kwa uzalendo
bila kuangalia dini zao na makabila yao.
Makonda
amesema kuwa kila mtu lazima ajiulize juu ya mashujaa katika kufanya
kazi katika kungalia kutenda haki pamoja na uzalendo kwa masilahi ya
taifa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka Ngao kwenye Mnara uliopo
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwakumbuka Mashujaa
waliopigana vita hapa nchini. Siku ya Mashujaa hufanyika Julai 25 kila
mwaka.
Askali
wakitoa heshima wakati wa sherehe za kumbukumbu ya mashujaa ambayo
imefanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wakati wa sherehe za
kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita hapa nchini.
No comments:
Post a Comment