Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, July 25, 2016

MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA YAMTIA HATIANI MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANAHABARI MWANGOSI

 
Msafala wa gari za FFU zilizomsindikiz askari mwenzao anayekutwa na kosa la kuua bila kukusudia leo
Askari wa FFU wakitoka mbio mahakamani hapo
Wananchi na wanahabari wakitoka mahakamani hapo
wakili kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki akizungumza na wanahabari nje ya viwanja vya mahakamani leo. 
 
Na MatukiodaimaBlog Iringa

MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imemtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa kumuua mwanahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi.

Huku wakili upande wa jamhuri katika kesi hiyo Adolph Mwaganda akiiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa askari huyo ambae hata hivyo alisema upande wa jamhuri hauna taarifa za makosa yoyote aliyopata kuyafanya.

Hata hivyo mahakamani hiyo imesema adhabu kwa mtuhumiwa huyo kutokana na kupatikana na kosa hilo la kuua bila kukusudia itatolewa Julai 27 majira ya saa 4 asubuhi mwaka huu.

Jaji Dkt Paul Kiwelo ambaye anayesikiliza kesi hiyo alisema mahakakamani hapo leo kuwa kati ya vielelezo vitano vyote vilivyoleta kama ushahidi mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo namba 54 ya mwaka 2013 ni kielelezo kimoja pekee cha ungamo kwa mlinzi wa amani ambacho ndicho hakukuwa na shaka na ungamo hilo ndilo lililomtia hatiani asikari huyo.

Alivitaja vielelezo vilivyopelekwa kama ushahidi kuwa ni Ramani ya eneo la tukio,ripoti ya tabibu ,ungamo la mlinzi wa amani ,silaha aliyoitumia na rejista ya silaha .

Hata hivyo alisema kuwa idadi ya mashahidi katika kesi sio inayowezesha kumtia hatiani mtuhumiwa ila kinachomtia hatiani ni aina ya ushahidi wenye uhakika ambao unatolewa na kuongeza kuwa katika kesi hiyo upande wa jamhuri ulishindwa kuleta mashahidi stahiki zaidi ya kuwa na mashahidi ambao ukiacha mlinzi wa amani mashahidi wote ushahidi wao una masahaka na haoonyeshi kama mtuhumiwa huyo ndio aliyehusika na mauwaji .


Askari hao wakimtoa mahakamani hapo leo mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi
Marehemu Mwangosi enzi za uhai wake
“ Niseme baada ya kusikiliza ushahidi wote …..mtuhumiwa kaonekana na kosa la kuua ila kujua kama alikuwa na nia ovu ama bila kukusudia ni jukumu la Jamhuri ambayo ilipaswa kuleta ushahidi ….. maelezo ya ungamo ambayo hata hivyo hayaonyeshi alipanga ila ni uzembe wa hali ya juu …..haijathibitika kuwa alikusudia mahakama inaamini hakukusudia”

Hivyo alisema kuwa mahakama yake imelifuta kosa la kuua kwa kukusudia na kumtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia alisema jaji Kiwele kuwa hamakama yake inashangazwa na RCO kwa kuleta mahakamani kesi ambayo ushahidi wake haukukamilika .

“ Ushahidi pekee ambao ni ule wa mlizi wa amani hakimu Flora Mhelela ambae kweli alitoa ushahidi usio na shaka hata kidogo ila ushahidi mwingine wote ulikuwa na mashaka mengi mfano ushahidi namba moja , mbili na nne ni ushahidi ambao haukuwa halisi “

Alisema mfano jambo la kujiuliuza katika ungamo lake mtuhumiwa lisema kuwa silaha aliyokuwa akitumika wakati amemzingira mwanahabari huyo ilifyatuka bahati mbaya hivyo ilikuwa ni mbovu ila cha kushangaza hakuna hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa silaha hiyo ilikuwa mbovu ama nzima.

Alisema kuwa si salama sana kumtia hatiani mtuhumiwa huyo kwa kosa la mauwaji ya kukusudia wakati upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi kamili unaoonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alikusudia kufanya mauwaji hayo.

Aidha alisema mbali ya upande wa utetezi pamoja na mtuhumiwa kukana ungamo alilolitoa Septemba 5 mwaka 2012 kwa mlinzi wa amani kuwa hakulitoa kwa uhuru na amani ila bado haisaidii kulikataa sasa maana kama si kweli alipaswa kielelezo hicho kukataliwa siku ya kwanza kilipofikishwa mahakamani hapo kama ushahidi hivyo mahakama hainashaka na kieelezo hicho amacho ni ungamo kwa mlinzi wa amani.

Simon ambae anatetewa na wakili wake Lwezaula Kaijage aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu sahihi yenye jicho la huruma kwa mteja wake huyo kwani hana wazazi na yeye ndio anategemewa na wadogo zake watano pia ana mtoto wa miaka mitano anayehitaji zaidi malezi yake katika makuzi yake.

“Mheshimiwa jaji huyu mshitakiwa ni kijana mdogo mwenye miaka 27 na ni nguvu kazi ya Taifa pia katika oparesheni hiyo ya Septemba 2 mwaka 2012 alikuwa katika kazi hiyo ambayo ilikuwa ni amri ya jeshi na kuwa slaha ililipuka bahati mbaya basi ijulikane hivyo pia amekuwa mahabusi miaka minne na kwa kipindi chote amekuwa akijutia kosa lake hilo…. Naomba anachiwe huru kwa masharti ambayo mahakama inaona yanafaa”

Huku wakili upande wa jamhuri katika kesi hiyo Adolph Mwaganda akiiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa askari huyo ambae hata hivyo alisema upande wa jamhuri hauna taarifa za makosa yoyote aliyopata kuyafanya.

“ Hatuna kumbukumbu ya kosa lolote ila kwa kuwa mahakama imemtia hatiani kwa kosa dogo la kuua bila kukusudia tunaomba mahakama yako kutoa adhabu kwa mujibu wa kifungu namba 198cha kanuni ya adhabu sura namba 16 mapitio ya mwaka 2002 kwamba mtu yeyote aliyetiwa hatiani kwa kosa la mauwaji ya bila kukusudia afungwe jela maisha “

Kesi hiyo ambayo ilijaza umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Iringa huku polisi wa FFU na wale wa kawaida wakitanda nje ya mahakama hiyo na ndani ya chumba cha mahakama kabla ya msajili wa mahakama hiyo kutoa onyo kwa jeshi la polisi kufuatia vurugu mbali mbali wanazozifanya mara kwa mara katika kesi hiyo , wakili kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki alisema kuwa hajapendezwa na nguvu kubwa ya jeshi la polisi ambayo wanaitumika katika kasi hiyo ndani na nje ya mahakama kuwa kinachofanyika ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Kwani alisema mahakama haipaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote na kuwa kitendo cha polisi kuzuia wanahabari ndani ya mahakama kufanya kazi zao kabla ya kesi kuanza ama baada ya kesi kumalizika si haki .

Lakini pia wakili msom I Ishabakaki, alisema kwa maoni yake anaona kulikuwa na mapungufu kwanzia kweye uchugunzi wa kesi ya mpaka uendeshaji wa kesi hiyo. Wakili msomi alisema anaunga mkono maswali ambayo mahakama ilijiuliza kwa nini RPC na RCO hawakuitwa kutoa ushaidi.

Wakili anasema kutkana na mwenendo wa kesi kwa kitendo cha viongozi wa juu kutokuita mahaakamani kuisaidia mahakama kunaweza kukawa kumepindisha haki sit u kwa marehumu mwangosi lakini hata kwa askari aliyehukuiwa.

Hii ni kutkana na kwamba mahakma iisema imepata kazi sana kutambua siku hiyo oda ilitoka kwa nani. 
 

Ulinzi wa polisi viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa leo kabla ya mtuhumiwa wa mauwaji kufikishwa
Wananchi wakiwa foleni kukaguliwa kabla ya kuingia mahakamani leo
Mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi akipakiwa kwenye gari za FFU 

No comments:

Post a Comment