MWENYEKITI WA WALEMAVU WA MACHO LUSIUS MLOWEZI AKIENDESHA MKUTANO WA WALEMAVU MKOA WA NJOMBE KWAMBA WAACHE OMBAOMBA INAWADHARIRISHA WALEMAVU WENGINE
AFISA USTAWI WA JAMII WA HALMSHAURI YA MJI WA NJOMBE HOSEA YUSTO AKIZUNGUMZA NA WALEMAVU HAO NA KUAHIDI KUWATAFUTIA FIMBO NYEUPE KWA WADAU WENYE MAPENZI MEMA NA WALEMAVU HAO
WALEMAVU WA MACHO WAKIWA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALEMAVU MKOA WA NJOMBE JACKSON FIHANGA AMBAYE NI MLEMAVU WA MIGUU ALIYEVAA BARAGASHIA NYEUPE AKISAIDIA KUANDIKA MIHTASARI
HII NI TIMU YA WALEMAVU WA MACHO MKOA WA NJOMBE WENGINE WAMETOKEA LUDEWA, WANGING'OMBE NA MAKAMBAKO
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA AFISA USTAWI WA JAMII WILAYA YA NJOMBE AVERINO CHAULA IGNASIA MFAUME AMETAKA WANANCHI KUTOWAFICHA WATU WENYE ULEMAVU KWANI NAO WANAHAKI KAMA WATU WASIYO NA ULEMAVU
Serikali Za Vijiji Na Kata Zimetakiwa Kuwatambua Watu Wenye Ulemavu Wa Viungo Mbalimbali Kwa Kuwapunguzia Tozo Za Michango Ya Utekelezaji Wa Miradi Iliyopo Kwenye Maeneo Yao Hususani Watendaji Wa Vijiji Ambao Wamekuwa Wakiwalazimisha Walemavu Kuchangia Michango Licha Ya Kutambua Ulemavu Wa Viungo Hivyo.
Wakizungumza Baadhi Ya Walemavu Wa Macho Wakiwa Kwenye Mkutano Wao Wamesema Wamekuwa Wakikabiliana Na Changamoto Mbalimbali Zikiwemo Za Kutozwa Michango Ya Utekelezaji Wa Miradi Kwa Lazima Hata Kama Hawana Uwezo Wa Kupata Fedha Hizo Na Kukosa Uwezo Wa Kufanya Kazi Ambazo Zinahatarisha Usalama Wao Kulingana Na Maumbile Walio Nayo.
Aidha Walemavu Hao Pia Wameomba Kupatiwa Vibali Vya Matibabu Bure Kwenye Zahanati Na Hospitali Kwani Wanashindwa Kupata Fedha Ya Kuchangia Mfuko Wa Taifa Wa Bima Ya Afya Na Kusababisha Wengine Kukosa Huduma Za Matibabu Kutokana Kukosa Fedha Za Matibabu Huku Walimu Wa Shule Za Msingi Na Sekondari Wakidaiwa Kuwanyanyasa Kwa Kufukuza Watoto Wao .
Lusius Mlowezi Ni Mwenyekiti Wa Walemavu Wa Macho Wilaya Ya Njombe Ambaye Pamoja Na Kutaka Serikali Iwashirikishe Walemavu Kwenye Vikao Vya Maamuzi Huku Walemavu Wakitakiwa Kuanzisha Vikundi Vya Kiujasiliamali Ikiwemo Ufugaji Wa Kuku Kwa Manufaa Yao Na Kuacha Kuomba Misaada Hovyo Mitaani.
Kwa Upande Wao Maafisa Ustawi Wa Jamii Wa Halmashauri Ya Mji Na Wilaya Ya Njombe Hosea Yusto Na Ignasia Mfaume Wamepongeza Walemavu Wa Njombe Kwa Kukemea Tabia Ya Kuomba Hovyo Misaada Kama Mikoa Mingine Na Kutaka Waungane Pamoja Ili Wawe Na Sauti Ya Pamoja Na Kuacha Kuwaficha Walemavu Nyumbani Badala Yake Wawashawishi Wajiunge Kwenye Chama Hicho.
No comments:
Post a Comment