Jumba la kifahari la mapumziko la Shirika la Ndege la Etihad Airways katika uwanja wa ndege wa Melbourne, Australia.
Shirika
la ndege la Etihad leo limefungua rasmi jumba jipya la kifahari kwa
ajili ya kupumzikia abiria wake katika uwanja wa ndege wa Melbourne,
Australia. Jumba hilo ni mahususi kwa kuwapatia abiria mazingira tulivu
ambayo wanaweza kupumzika, kuongeza nguvu, kula, kufanya kazi au
kuburudishwa kabla ya safari.
Ni
eneo ambalo limejawa na nuru ya asili yenye vioo tokea sakafuni hadi
katika dari, inatoa mtazamo mpana wa eneo la kurukia ndege. Lina zaidi
ya mita za mraba 800 yenye viti vya kukaa hadi kufikia wageni 133, ni
nyumba ya kupumzika ya shirika la ndege la Etihad ambayo ni kubwa zaidi
iliyoko nje ya Abu Dhabi.
Sehemu
ya katikati ya nyumba hii ya kupumzika ni eneo la kulia chakula lenye
viti 26 vya ukaribu. Sehemu hii wageni watafurahia alama ya ukarimu ya
shirika hili kwa kula katika Mgahawa unaotoa huduma ya chakula cha pekee
na buffet la kimataifa.
Wapishi
wenye ujuzi wa hali ya juu huwepo pale muda wote wakipika kila chakula
kwa kutumia bidhaa za msimu zilizokusanywa kwa njia ya kawaida. Hii
inajumuisha mikate freshi ambayo inaokwa kila siku mara mbili, Grissini
bradstick; ya kuchovya kama vile humus, Baba ghanoush na muhammara;
piko; labneh; biskuti; na hata ice cream, Jibini, matunda na mboga za
majani zinachukuliwa kutoka Victoria suppliers na kahawa inatoka kwa
wakaangaji wa kahawa wa Melbourne.
Sifa
nyingine ya kipekee ni bar yenye picha za vinyago, iliyojaa mvinyo
kutoka kwa watengenezaji wa Victoria na zaidi ya aina 70 ya vinywaji
bora vikali, shamapeni na viamsha hamu. Muongozo wa kuagiza Cocktail pia
unapatikana. Uchaguzi wa kibunifu, umetengenezwa kwa ushirikiano na
washauri wa mambo ya vinywaji wanaoongoza kutoka London Fluid Movement,
inajumuisha aina ya kipekee ya Cocktail yenye majina ya vituo mbalimbali
kama Melbourne, Sydney, Paris na New York na Mock tail inayoitwa Abu
Dhabi, Controlled Airspace na Winglet. Cocktail na Mock tails ya
Controlled Airspace na Winglet. Kama ilivyo kwa vyakula vilivyoko katika
orodha ya mwongozo iliyoko katika sehemu ya chakula, zote
zimetengenezwa kwa mkono kwa kutumia wachanganyaji waliopitia mafunzo,
wakitumia syrup na garnishes kama vile Candy floss na rhubarb
zilizokaushwa ambazo zimetengenezwa ndani ya jumba hili na wataalamu wa
jadi, bar inatoa uchaguzi wa kisasa, kama vile Mach 10 Majito, ambayo
imegunduliwa na kutengenezwa na Fluid Movement. Wapenzi wa Negroni
watafurahia kufahamu kuwa kiamsha hamu kimechanganywa, kikavundikwa na
kuhifadhiwa nyuma ya bar.
Ubunifu
wa ndani, kanuni ya mtindo, nafasi na utulivu vimekamilishwa na shirika
la ndege la Etihad kutoka kwenye bidhaa zake za kipekee za ‘Facets of
Abu Dhabi’ ikiwa na mtindo wake wa kijiometri na rangi ambayo inapewa
motisha na mandhari ya UAE, ni mwonekano wa kipekee wa karne ya 21 ya
ubunifu wa Abu Dhabi.
Fanicha
za kitamaduni – zilizoandaliwa na Boss – zinawapatia wageni wa nyumba
hii ya kupumzika uchaguzi wa mtindo wa kukaa, kila mmoja imebuniwa
kwaajili ya kuongeza kiwango cha starehe na utulivu wakati wa kula,
kufanya kazi na kupumzika.
Pamoja
na kuanza kwa huduma za A380 tokea tarehe 01 Juni, wageni katika daraja
la makazi watafurahia upekee wa nyumba ya kupumzikia ya binafsi –
ambayo imejengwa kwa makini kabisa kando ya lango kuu la kuingilia
katika jumba la mapumziko. Ikiwa na viti vyenye mikono iliyofunikwa kwa
ngozi ya Kiitalia ya Poltrona Frau, vilivyokamilishwa kwa vitambaa safi
laini vya mahameli, chumba cha peke yake cha kupumzika na mlango wa
kujitegemea, Nyumba ya kupumzika ya Daraja la Makazi ina huduma za
kuagiza za kitajiri na huduma binafsi ambazo zinalingana na ukarimu wa
kiwango cha juu wa shirika hili la ndege.
Huduma
nyingine katika Nyumba kuu ya kupumzikia inajumuisha vyumba tofauti vya
kupumzika kwa ajili ya wanawake na wanaume vyenye mabafu pamoja na
bidhaa za Scaramouche + Fandago, vyumba maalumu vilivyotengwa kwaajili
ya wanawake na wanaume kuchukulia udhu na vyumba tofauti vya kuswalia na
chumba cha watoto kucheza na chumba cha mizigo.
Huduma ya Wi-Fi yenye kasi inakamilishwa na soketi za umeme ambazo zimewekwa kila mahali katika Nyumba ya kupumzikia.
Makamu
wa Rais katika Idara ya Masoko wa Shirika la ndege la Etihad bwana
Shane O’Hare, aliyekata utepe wa sherehe akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
shirika la ndege la Melbourne bwana Lyell Strambi katika ufunguzi rasmi
leo alisema:
“Nyumba
mpya ya kupumzika ya kifahari iliyoko Uwanja wa ndege wa Melbourne ni
daraja la peke yake – ni nyumba ya kupumzikia ya uwanja wa ndege kama
ambavyo inajulikana, ambayo imeboreshwa kabisa.
“Ikiunganisha
Mgahawa bora wa chakula na Bar ya Cocktail, Nyumba hii ni maonesho ya
ubunifu wa kiwango cha juu na umakini ambao wageni watafurahia kiwango
cha juu cha utulivu na starehe, inayokamilishwa na ukarimu wetu wa
kiwango cha kimataifa, ubunifu katika mapishi na teknolojia ya kiwango
cha juu ya vinywaji.
“Wakati
huo huo, inakuletea hisia kali ya kitamaduni kwa jibini freshi na
mvinyo – unaochukuliwa kutoka kwa wakulima, watengenezaji na wasambazaji
katika jimbo lote la Victoria – ambayo inawapatia wageni wetu ladha ya
kusisimua ya utamaduni na umaarufu wa upishi.
“Ufunguzi
wa huduma hii ya kustaajabisha na uzinduzi wa huduma yetu kuu ya A380
hapo tarehe 1 Juni, unawapa wageni wetu katika ruti ya Melbourne na Abu
Dhabi uzoefu wa ushawishi wa huduma ya hali ya juu kuliko zote.”
Wageni
katika Makazi, Apartments za kwanza na Business Studios watakaribishwa
kutembelea Nyumba ya kupumzikia kabla ya kusafiri. Wanachama wa
Platinum, Dhahabu na Fedha wa wageni wa Etihad na wanachama wenye sifa
wa mashirika ya ndege washirika wa shirika la ndege la Etihad na mpango
wa Uaminifu (loyalty) wa mashirika ya ndege washirika wataweza kutumia
nyumba hii ya kupumzika wanapokuwa wanasafiri katika Daraja la Economy.
Wageni lazima wawe ameorodheshwa katika ndege ya shirika la ndege la
Etihad inayofanya kazi siku hiyo.
Iko
katika kituo cha 2 karibu na lango la 10, nyumba ya mapumziko itakuwa
wazi takribani masaa matatu kabla ya kuondoka kwa ndege za Etihad mara
mbili kila siku katika ruti ya Melbourne kwenda Abu Dhabi.
Jumba
hili linaongeza orodha inayokuwa ya nyumba za kiwango cha juu za
kupumzikia zilizoko Sydney, Abu Dhabi, Dublin, Frankfurt, London
Heathrow, Manchester, Paris, Washington DC na New York. Njumba ya
kupumzikia ya daraja la kwanza iliyoko katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Abu Dhabi na Jumba jipya la kupumzikia la daraja la Kwanza
na business huko Los Angeles yatafuata miezi ijayo.
Shirika
la ndege la Etihad lilianza safari za ndege za kila siku kwenda
Melbourne mwezi Machi mwaka 2009. Leo, inafanya safari zake mara mbili
kila siku, safari zisizo na ukomo kwenda Abu Dhabi na nje ya GCC, Afrika
na Ulaya. Ni shirika pekee la ndege linalotoa safari zisizo na ukomo za
kila siku kutoka Melbourne kwenda katika Umoja wa mataifa ya Kiarabu.
Wabebaji wa bendera ya UAE watatambulisha ndege yao kuu ya A380 hapa
Melbourne kuanzia tarehe 1 June 2016, jambo ambalo litaleta daraja la
Makazi katika ruti hii, vyumba vitatu vya peke yake katika ndege ya
kibiashara duniani.
Zaidi
ya kufanya safari zake mara mbili kila siku kwenda Melbourne, Shirika la
ndege la Etihad inafanya safari zake za kila siku kwenda Brisbane na
kwenda Perth na huduma 11 kwa wiki kwenda Sydney. Mashirika ya ndege
washirika ya usawa, Virgin Australia, inafanya safari zake tatu nyingeza
za kila wiki kati ya Sydney na Abu Dhabi.
No comments:
Post a Comment