WAFANYAKAZI WAKIWA KWENYE MAANDAMANO SIKU YA MEI MOSI MJINI MAKAMBAKO
SKAUTI WAKIWA IMARA WAKATI MGENI RASMI AKITOA HOTUBA SIKU YA MEI MEI MOSI
KIKUNDI CHA NGOMA KUTOKEA MWEMBETOGWA WAKITO BURUDANI YA NGOMA YA ASILI
MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIWA JUKWAANI KUHUTUBIA SIKU YA MEIMOSI
HAPA ANAWAAPISHA WAFANYA KAZI WOTE KUWA WAADILIFU
Jumla Ya Watumishi Hewa 108 Wameisababishia Serikali Hasara Ya Zaidi Ya Shilingi Milioni Mia Tatu Katika Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Ambapo Jitihada Za Kuwabaini Watumishe Hewa Wengine Bado Zinaendelea Na Kutaka Ushirikiano Ufanyike Baina Ya Vyama Vya Wafanya Kazi Na Serikali Kuwabaini Watumishi Hao Wasiyostahili.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Kwenye Maadhimisho Ya Sikukuu Za Wafanyakazi Mei Mosi Ambayo Kwa Mkoa Wa Njombe Yamefanyikia Katika Uwanja Wa Polisi Makambako Na Kubainisha Watumishi Hewa Mia Moja Na Nane Ambao Wameisababishia Serikali Hasara Ya Jumla Ya Shilingi Milioni Mia Tatu Tisini Na Mbili Na Laki Nane.
Aidha Dkt Nchimbi Amekiagiza Chama Cha Wafanya Kazi TUCTA Kwa Kushirikiana Na Vyama Vingine Vya Wafanyakazi Kuhakikisha Vinapeleka Majina Ya Watumishi Hewa Ambao Wapo Kwenye Vyama Hivyo Ndani Ya Mwezi Mmoja Nakwamba Wafanya Kazi Wamekuwa Wakilalamikia Serikali Kuwatekelezea Mahitaji Yao Huku Baadhi Yao Ni Watumishi Hewa Bila Kuwaondoa Kwenye Mfumo Wa Ajira Serikalini .
Katika Hatua Nyingine Dkt Nchimbi Amekitaka Chama Cha Wafanyakazi TUCTA Kuwatembelea Wahudumu Wa Kwenye Biashara Za Bar Kuhakikisha Wanapewa Mikataba Na Waajili Wao Agizo Ambazo Linatakiwa Kutekelezwa Kwa Kipindi Cha Miezi Mitatu Pamoja Na Kuwatembelea Wafanyakazi Wengine Kubaini Matatizo Yanayowakabili.
Wakizungumza Na Uplands Fm Mara Baada Ya Hotuba Ya Mgeni Rasmi Baadhi Ya Wafanyakazi Wa Mashambani Wameipongeza Serikali Kwa Kuhimiza Waajili Kuwalipa Ujira Unaotakiwa Watumishi Wa Sekta Mbalimbali Zikiwemo Sekta Binafsi Huku Wakisema Waajili Wengi Wamekuwa Wakiwakandamiza Wafanyakazi Wao Kwa Kuwalipa Ujira Mdogo.
Katika hatua nyingine Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amezitaka Halmashauri Za Mkoa Huo Kutenga Maeneo Kwaajili Ya Viwanja Vya Kujenga Nyumba Za Watumishi Kwa Kuwatoza Fedha Kidogo Kuliko Kuwapangishia Nyumba Zisizo Na Hadhi Na Kuchukua Kodi Jambo Ambalo Limetajwa Kuwa Ni Kuwakandamiza Watumishi Hao.
Dkt Nchimbi Ametaka Halmashauri Hizo Kutekeleza Agizo Hilo Kwa Wakati Mara Viongozi Watakapo Kutana Ili Watumishi Waweze Kujenga Nyumba Zao Na Kuimarisha Uchumi Kwa Kulima Mashamba Kwaajili Ya Matunda Aina Ya Parachichi.
Aidha Dkt Nchimbi Amesema Kuanzia Sasa Kila Mtumishi Mahala Anakoishi Anatakiwa Kuwa Na Miti Ya Matunda Aidha Ya Parachichi Kwaajili Ya Manufaa Ya Familia Zao Na Kukuza Uchumi Wa Kila Mmoja Hatrua Ambayo Itahamasisha Wananchi Wengine Kuiga Mfano Huo Na Kuanzisha Kilimo Cha Matunda Huku Akiagiza Kila Shule Kuwa Na Ekari Moja Ya Zao La Matunda Hususani Parachichi.
Dkt Nchimbi Amewaagiza Makatibu Tawala Wote Wa Wilaya Na Mkoa Kuhakikisha Wanawachukulia Hatua Kali Za Kisheria Watumishi Wote Wanaokwenda Kunywa Pombe Kwenye Bar Na Virabu Na Kusema Baadhi Ya Biashara Za Bar Zinatuhumiwa Kwa Kuhusika Kuwauza Wasichana Kingono Jambo AMbalo Linatakiwa Kukemewa Na Kila Mmoja.
Dkt Nchimbi Amezungumzia Uchumi Utakao Kuwepo Mara Machimbo Ya Chuma Cha Liganga Na Makaa Ya Mawe Kwenye Mgodi Wa Mchuchuma Wilayani Ludewa Ambapo Wananchi Wanatakiwa Kuwekeza Zaidi Kwenye Ufugaji,Kilimo Cha Matunda,Mbogamboga,Mahindi Na Mazao Mengine Kwaajili Ya Kuinua Uchumi Wao Ikiwemo Ufugaji.
Katika Kutekeleza Kauli Mbiu Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Rehema Nchimbi Ya Kwamba Njombe Ni Lango Kuu La Uchumi, Baadhi Ya Wakulima Wameanza Kutekeleza Kauli Hiyo Akiwemo Daitan Mhema Mkazi Wa Kijiji Cha Matiganjora Ambaye Ana Ekari Takribani Tano Za Matunda Aina Ya Parachichi.
Maadhimisho hayo kwa siku ya leo yamebeba ujumbe usemao DHANA YA MABADILIKO ILENGE KUINUA HALI ZA WAFANYA KAZI.
No comments:
Post a Comment