Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni
hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa
jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka
Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP
Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo
Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Msanii
huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga ‘Live Music’
katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini,
Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama,
Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi
watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
Msanii
wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa
safari ya Mwanza.
Msanii
wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum
aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO
Motors Group.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa
Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika
la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016
mara baada ya kutua jijini Mwanza. Kampuni ya simu mkononi Vodacom
Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana
na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK
Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe
Media Group pamoja na Coca Cola.
Baadhi
ya wapiga vyombo waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka
kwenye ndege ya shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini
Mwanza jioni. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini
wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la
Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF
Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na
Coca Cola.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla
(wa pili kushoto) na Mwanakamati ya Jembeka Festival 2016, Sharon
wakiwasili na katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016,
Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja
na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika
picha ya pamoja.
Balozi
wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement
akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,
Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.
Msanii
wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-‘show love’ na Balozi wa
Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement
aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai. Kampuni ya
simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival
2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP
Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo
Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM.
Msanii
wa kikundi cha ngoma cha Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza
akimshikisha nyoka aina chatu msanii wa kimataifa kutoka nchini
Marekani, Neyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakiwemo wa JEMBE FM wakifanya mahojiano na msanii Neyo alipowasili jijini Mwanza.
Wakazi
wa jijini Mwanza wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha
waliofika kumlaki katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.
Mwanasheria
wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa
kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana
mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa
kutumbuiza kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment