Mkuu
wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha ameagiza maafisa tarafa
kusimamia kwa karibu shughuli za hifadhi ya mavuno yaliyopatikana katika
Mvua za vuli Msimu wa 2015/2016 kwa kuhamasisha wananchi wenye
mavuno mengi kila mahali kuhifadhi vizuri ili mavuno hayo yasiharibike
na kuweka akiba ya kutosha kwaajili ya kaya zao.
Pia
ameagiza Wakulima washauriwe kuuza ziada tu ya mavuno yao kwaajili ya
kukidhi mahitaji yao muhimu na kila kaya isimamiwe kuhakikisha
imehifadhi mazao ya chakula cha kuwatosha huku akiagiza Wafugaji
washauriwe kuvuna sehemu ya mifugo yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao
muhimu na kununua nafaka kwaajili ya kaya zao.
Amesisitiza
maelezo haya yawafikie viongozi ngazi za kata,vijiji na vitongoji
kwaajili ya utekelezaji na taarifa iwasilishwe kwa Mkuu wa Wilaya kabla
ya 13/05/2016.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita
06 Mei, 2016
No comments:
Post a Comment