Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Juliana Pallangyo (pichani) akisoma hotuba ya ufunguzi wa
mkutano wa siku tatu jijini Dar es Salaam uliokutanisha wataalam
kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam
mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani
Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro
nchini Uganda.
Wataalam
mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Juliana Pallangyo ( anayeonekana mbele kwa mbali)
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Juliana Pallangyo (wa nne kutoka kushoto waliokaa mbele)
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya
ufunguzi.
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Imeelezwa
kuwa Tanzania inatarajia kuzalisha megawati 100 ndani ya kipindi cha
miaka saba ijayo na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana
Pallangyo katika mkutano uliokutanisha wataalam kutoka nchi mbalimbali
kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti
uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna
viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.
Wataalam
katika mkutano huo ulioandaliwa na Kampuni ya Maendeleo ya
Jotoardhi Tanzania (TGDC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje
Iceland, wanatoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda,
Ethiopia, Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu Dk. Pallangyo alisema kuwa
kutokana na ugunduzi wa nishati ya jotoardhi nchini Tanzania,
serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ndani ya kipindi cha miaka
saba ijayo inazalisha megawati 100 zitakazoongezwa kwenye gridi ya
taifa na hivyo kupunguza tatizo la upungufu wa umeme nchini.
Alisema
kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa nishati ya umeme
inachangia katika ukuaji wa uchumi na kupelekea nchi kutoka kwenye
orodha ya nchi masikini duniani na kuingia katika nchi zenye kipato cha
kati ifikapo mwaka 2025, kama Dira ya Maendeleo ya Taifa
inavyofafanua.Aliongeza kuwa kuwepo kwa nishati ya uhakika kutavutia
uwekezaji kwenye viwanda na kuzalisha ajira na nchi kupiga hatua
kimaendeleo.
Alisisitiza
kuwa Tanzania ina nishati ya kutosha ya jotoardhi yenye uwezo wa
kuzalisha umeme wa megawati 5000 ambayo haijatumika bado ambapo serikali
imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Kampuni
ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Aliendelea
kusema kuwa TGDC ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia
maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania na kuanza rasmi shughuli zake
Julai 2014 jukumu lake kuu likiwa ni kutafiti, kuchimba na kutumia
rasilimali za jotoardhi kwa uzalishaji umeme na matumizi mengine ya moja
kwa moja.
No comments:
Post a Comment