Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akizungumza na
waandishi wa habari jijini Mbeya (Hawapo pichani)katika kuzngumzia
tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu
katika duka la kuuzia vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya
Mkoani Mbeya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina
ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo
ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya
uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi
Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina
ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao .
Baadhi ya
askari polisi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kaimu kamanda wa
Polisi Mkoa wa mbeya Butusyo Mwambelo wakati akizungumza na waandsihi wa
habari kufuatia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu waliotaka kufanya
uhalifu katika duka la vinywaji vya jumla linalomilikiwa na ndugu
Hamisi Mkazi wa Matundasi Chunya Mkoani Mbeya .
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.
Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya).
JESHI la
Polisi mkoani Mbeya limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi wakati wa kurushiana rasasi.Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Butusyo Mwambelo amesema tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu
saa 2 usiku , huko katika kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani
Mbeya .
Amesema
watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya
aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ,
walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya uhalifu kwenye duka la
jumla la kuuzia vinywaji mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa eneo hilo la
Matundasi Chunya..
Kamanda
Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha
mochwari katika hospitali ya wilaya ya Chunya , majina na makazi yao
bado hayajajulikana.Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia
wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye
eneo la tukio.
“Baada ya
polisi kufika katika eneo la tukio watu hao walistuka kuwa
wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji
cha Matondo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761. AFS
aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo .Amesema walipoona
Polisi wanawakaribia walianza kurusha risasi hovyo hewani ambapo
jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na
kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa kutoroka .
Amesema
kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi lilianzisha msako usiku huo
na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili ambao huku wengine
wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu
hao.Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana bunduki moja aina ya SMG
yenye namba 1996 AFU 1120 ikiwa na risasi 27 kwenye magazine. Pia
pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana
pamoja na panga .
Mwambelo
alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua
watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya
uhalifu sanjali na kufika katika hospital ya wilaya ya Chunya kwa lengo
la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao kwani majina yao bado
hayajatambulika.
No comments:
Post a Comment