Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, March 25, 2016

WAKRISTO WATAKIWA KUWATHAMINI MAPADRE KULETA MAENDELEO YA KIROHO MAHALI PA KANISA

 MUHASHAMU ASKOFU ALFRED  MALUMA  JIMBO LA NJOMBE LEO AMEONGOZA MISA YA IJUMAA KUU AMBAPO JANA ALIONGOZA MISA YA ALHAMISI KUU


Mhashamu Askofu Wa  Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Alfred Maluma Amewataka Wakristo Kudumisha Upendo Katika Kipindi  Cha Skukuu Na Kuwa Na Roho Ya Kujitoa Katika  Kusaidia  Wasiyojiweza ,Kutemkbelea Wagonjwa Na Kwenye Huduma Za Kiroho  Ili Kuonesha Upendo  Na Ukristo  Kwa Jamii Yote.

Akizungumza Wakati Akiongoza Misa Ya Siku Ya Maadhimisho Ya Alhamisi Kuu   Muhashamu  Askofu Maluma  Amesema Katika Injili Iliyosoma Siku Ya Jana  Yesu Kristu Anawaosha Mitume Na Kusisitiza Huduma Ya Upendo  Kwa Mapadre,Wakristo Na Watu Wengine  Ambao Kristo Amewakusanya Ili Wapate Huduma Ya  Mungu.

Aidha  Askofu Maluma Amesema  Kuna Umuhimu Wa Mapadre Kuwepo Katika  Kanisa  Kwamba Ni Kristo Mwingine  Ambapo Siku Hiyo Ya Alhamisi Kuu Ni Skukuu Ya Mapadre   Ambayo Inaambatana Na Kutoa Huduma Ya Kutakasa Inayoweza Kuambatana Na Huduma Nyingine Za Kibinadamu  Kwaajili Ya Kukamilisha Na Kutafsili Sura Halisi Ya Upenda.

Muhashamu Askofu Maluma Amesema  Mapadre  Kwa Siku Za Alhamisi Kuu Wanatakiwa Kuwa Katika Maeneo Yao Ya Kutolea Huduma  Za Kiroho  Kwa Waumini   Na Kutoa Huduma Ya Kutakasa Ya Sakramenti Ya Wokovu  Ambapo Amesema Kigango  Ambacho Padre Yupo Maendeleo Yatakuwepo Kutokana Na Moyo Wito Wa Kuarika Watu Waamini Uwepo Wa Kristo.

Hata Hivyo  Askofu Huyo Amewaomba Wakristo Kuthamini Mapadre,Kuthamini Kanisa  Na Mafumbo Mbalimbali Ili Kuleta Wokovu Huku Wakitakiwa Kuwaombea Mapadre Wote  Wafanye Kazi Vizuri Na Kutaka Mapadre Nao Wawe Wanyenyekevu Kila Siku   Na Watambuwe Kwamba Wanabemba Dhamana Ya Kanisa.



No comments:

Post a Comment