Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, March 31, 2016

WABUNGE WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kangi Lugola (Mbunge wa Mwibala), Mh. Sadiq Murad (Mbunge wa Mvomero) pamoja na Mh. Victor Mwambalaswa (Mbunge wa jimbo la Lupa) wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, kwa kusikiliza kesi inayowakabili ya kushawishi kupatiwa rushwa ya Mil. 30 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja hapa nchini. 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

 WABUNGE watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuomba  rushwa ya sh.milioni 30.

Wabunge waliofikishwa Mahakama ya Kisutu leo ni Mbunge wa Mvomero, Sadiq Murad, Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, pamoja na Mbunge wa Mwibara Alphaxaid Kangi Lugola.

Mwendesha Mashitaka wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahela Ndimbo mbele Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,  Thomas Simba amesema tukio hilo lilitokea  Machi 15 mwaka huu  majira saa 2  had saa 4 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Ndimbo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa wajumbe Kamati Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) waliomba  rushwa ya sh.milioni 30 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana  Magota.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,Thomas Simba alidai kuwa upande wa mashitaka upeleke ushaidi  wa watuhumiwa wa rushwa .

Washitakiwa waliposomewa shitaka la kuomba rushwa wote walikana na dhamana yao kuwa wazi kwa masharti ya kila mmoja kwa na mdhamini wa mmoja wa sh.milioni tano pamoja na hati ya kusafiria ambapo wote walikidhi masharti ya dhamana hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ameairisha kesi hiyo mpaka Aprili 14 mwaka huu itakapotajwa tena .

No comments:

Post a Comment