RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyi Haji
Makame mara baada ya kuwasili Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya sherehe za
kuapishwa Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono mamia ya wananchi wa Zanzibar mara baada ya kuwasili katika
uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa
wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa kwa Rais wa awamu ya saba wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan
Kisiwani Zanzibar.
Gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na usalama vikiimba wimbo wa Taifa kwenye uwanja wa Amaan.
Rais
mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
akihutubia mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Amaan
Kisiwani Zanzibar mara baada ya kuapishwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai katika
uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani
Abeid Karume katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja
wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed
Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja
na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jeneral Devis Mwamunyange
wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na Yamoto bendi katika uwanja
wa Amaan.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika
uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja
na viongozi wengine wa Serikali wakifatilia kwa makini burudani
iliyokuwa ikitolewa na Bendi ya muziki ya Yamoto katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiondoka katika uwanja wa Amaan mara baada ya kumalizika kwa sherehe za
uapisho.
No comments:
Post a Comment