MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA ILEMBULA KWAAJILI YA KUSAFIRISHWA KESHO MACH 23 KWAAJILI YA MAZISHI DAR ES SALAAM
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Bi. Sarah Dumba katika picha enzi za uhai wake. .................................................................................... Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sara Dumba Amefariki Baada ya Kuugua Ghafla Jana Jioni
Akitoa Taarifa za Kifo cha Mkuu wa Wilaya Hiyo , Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi Amesema Marehemu Amefariki Wakati Akiendelea na Matibabu Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe (Kibena).
Kwa Mujibu wa Dkt.Nchimbi Amesema Kuwa Marehemu Sara Dumba Alifanya Kazi Zake
Kama Kawaidi Siku Nzima Hadi na Aliporejea Nyumba na Kupata Chakula, na Kwamba Mara
Baada ya Kupata Chakula Hali Ilibadilika na Kuanza Kutapika Huku Akilalamika Kukosa Hewa
Ambapo Alipelekwa Hospitali Majira ya Saa 1:20 na Kufariki Wakati Akipatiwa Matibabu.
Dkt. Nchimbi Amesema Taratibu za Mazishi Bado Zinaendelea na Kwamba Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Njombe Inakutana Leo Asubuhi Kupanga Ratiba Kamili.
Wakizungumza Na Waandishi Wa Habari Baadhi Ya Viongozi Wa Dini Waliofika Nyumbani
Kwa Marehemu Wamelezea Namna Walivyokuwa Wakishirikiana Na Aliyekuwa Mkuu Wa
Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba Wakati Wa Uhai Wake Kwamba Alihimiza Utekelezaji Wa
Miradi Ya Maji Na Kuwaunganisha Watumishi Wa Mungu Pasipo Kubagua Kanisa. Kabla ya Kuteuliwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Marehemu Sara Dumba Alikuwa Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania
Jamaa na Familia ya Marehemu Sara Dumba Pamoja na Uongozi wa Wilaya ya Njombe Hasa Katika Kipindi Hiki cha Majonzi.
Mungu Alitoa na Mungu Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe, Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Ma Hali Pema Peponi , Amen
No comments:
Post a Comment