………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof.Jumanne Mghembe amemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Huduma za Misitu nchini, (TFS) Bw. Juma Mgoo pamoja na Wakurugenzi
wawili wa wakala hiyo ili kupisha uchunguzi kutokana na ukusanyaji
usioridhisha wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu.
Prof. Maghembe ametaja majina ya
Wakurugenzi hao aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkurugenzi Rasilimali
Misitu, Bw. Zawadi Mbwambo pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango
na Matumizi endelevu ya Misitu, Bw. Nurdin Chamuya
Wengine waliosimamishwa kazi ni
wakuu wa Kanda za Wakala wa Huduma za Misitu nchi nzima ambao ni
Bw. Hubert Haule wa Kanda ya Kusini, Bw. Bakari Rashidi wa kanda ya
Mashariki, Bw. Shabani Mwinyi Juma wa kanda ya kati , Emanuel Minja wa
kanda ya Magharibi pamoja na Bw. Bruno wa nyanda za juu kusini
Akizungumza leo na Waandishi wa
Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, Prof. Maghembe
amesema hatua hiyo imekuja baada ya kubaini shehena kubwa za magogo
aina ya mninga katika Mkoa wa Rukwa wilayani Kalambo yakiwa
yamekatwa na kuwekwa ndani ya makontena kule kule ndani ya msitu
pamoja na kutengenezewa nyaraka feki zinazoonesha magogo hayo yanatoka
nchini Zambia tayari kwa kusafirishwa kupelekwa nchini China
lakini hata hivyo baada ya kubaini wizi huo hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania ( TFS).
Amesema kuwa baada ya kubaini
hivyo usiku wa jana aliweza kupata taarifa kuwa shehena ya Magogo hayo
yenye thamani ya shilingi milioni 500 yaliyotakiwa kupelekwa Makao
makuu ya Wilaya ya Kalambo yamemwagiwa petrol na yamechomwa moto
Aliongeza kuwa kumekuwa na
ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali
yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa
kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Kwa upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki zimekuwa zikipelekwa pungufu na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.
Kwa upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki zimekuwa zikipelekwa pungufu na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.
Wakati huo huo, Waziri Maghembe
amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Wanyamapori wa
Matumizi Endelevu, Dkt. Charles Mulokozi kwa kosa la kukaidi agizo la
kusaini vibali vya kusafirisha Wanyamapori nje ya nchi.
Hatua hiyo imekuja baada ya
jana nyani 61 kukamatwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro na kubaini kuwa Idara ya Wanyamapori ndio iliyotoa vibali
vya kusafirisha nyani hao na vibali hivyo vikiwa vimetiwa saini na
Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa ndege ya kutoka
Ulaya Kusini iliyotakiwa kusafirisha nyani hao imeshikiliwa pamoja na
rubani wake kwa mahojiano zaidi.
Prof ,Maghembe amesema kutokana
taarifa alizozipata kuwa jumla ya nyani 450 ndio waliokuwa wanawindwa
kwa ajili ya kusafirishwa kupelekwa nje.
No comments:
Post a Comment