Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, March 23, 2016

ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA KUSINI JAPHET MENGELE LEO ANATARAJIA KUONGOZA IBADA YA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA KUANZIA SAA SITA MCHANA WA LEO



Saraha Dumba

 MAREHEMU SARAH DUMBA  ENZI  ZA UHAI WAKE  ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE KUHUSIANA NA  WAKULIMA KUONGEZA KASI YA KILIMO CHA CHAI NJOMBE IGOMINYI.
 MKUU WA MKOA WA NJOMBE  DKT REHEMA NCHIMBI AKIZUNGUMZA  HII LEO OFISINI KWAKE JUU YA KIFO CHA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE  MAREHEMU SARAH DUMBA
 
 Askofu Wa Kanisa La Kiinjili La Kiluthel Tanzania KKKT Diosisi Ya Njombe Japhet Mengele Leo Anatarajia Kuongoza  Ibada Ya Kuuaga Mwili  Wa Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba  Ambaye Amefariki Ghafra  Mnamo Mach 21 Akiwa Katika Hospitali Ya Kibena Na Mwili Wake Kupelekwa Katika Hospitali Ya Ilembula Kwaajili Ya Kuhifadhiwa.

Kwa Mujibu Wa Taarifa Iliyotolewa Na  Richard Moshi  Kwa Niaba Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Jackson Saitabahu  Imeeleza Kuwa  Mwili Wa Marehemu Sarah Dumba Unatarajia Kusafirishwa Kutoka Katika Hospitali Ya Ilembula  Hadi Nyumbani Alikokuwa  Anaishi Marehemu  Ikulu Ndogo Kuanzia Majira Ya  Saa Nne Hadi Saa Tano Na Dakika Hamsini.

Bwana Moshi Amesema  Baada Ya Mwili Huo Kuwasili Nyumbani Mchangaji Ataongoza  Sara Fupi  Kisha  Washiriki  Watapata Chakula Cha Mchana  Na Baada Ya Hapo  Mwili  Huo Utapelekwa  Katika Kanisa La KKKT Diyosisi Ya Kusini  Kwaajili  Ya Ibada Ya Kuuaga Mwili Wa Marehemu.

Akizungumza   Ofisini Kwake Mkuu Wa Mkoa  Wa Njombe  Dkt Rehema Nchimbi   Amesema Marehemu Sarah  Philip Dumba   Enzi Za Uhai Wake Alikuwa  Mwanafamilia Wa Familia Nyingi  Nakwamba  Machi 21  Alikwenda Kazini    Na Hakukuwa na Taarifa Zozote Za Kuumwa Kwake  Ambapo Baada Ya Kufika Nyumbani Kwake Na Kula  Chakula   Muda Mfupi Alianza Kutapika Na Kulalamika Kukosa  Hewa.

Kwa Upande Wao Viongozi Wa Dini Mjini Njombe Wakiongozwa Na  Mchungaji Wa Kanisa La TAG Melinze Njombe  Mch.Cefania Tweve  Wameelezea Namna Walivyoshirikiana  Na Marehemu Mkuu Wa Wilaya  Ya Njombe Sarah Dumba Kwamba Alihimiza Utekelezaji Wa Maendeleo Pamoja Na Kuwaunganisha Wachungaji  Wote Pasipo Kujali Kanisa Gani.

Baadhi Ya Wananchi Na Viongozi Wa Siasa  Wamesema  Marehemu Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba Alikuwa Ni Kiongozi Ambaye  Ni Mchapa Kazi  Na Aliyependa Kuzungumza Na Kila Mmoja  Huku Wakisema Kifo Cha   Sarah Dumba  Kimeacha Pengo Kubwa Ambalo Halitazibika.

Rais Dkt. John Magufuli Amemtumia Salam za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi Kufuatia Kifo cha Ghafla cha Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sara Dumba Kilichotokea Machi 21 , 2016 Katika Hospitali ya Mkoa Huo (Kibena) Majira ya Saa Moja Usiku.

Mungu Alitoa na Mungu Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe, Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Ma Hali Pema Peponi , Amen
 

No comments:

Post a Comment