AWAMU YA TATU YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWAJILI YA KUMKOMBOA MWANAMKE WA KITANZANIA YAANZA DAR
Awamu
ya Tatu ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanza
leo. Wanawake 35 wa jiji la Dar es salaam Watanufaika na mafunzo ya
ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo
yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Felix Maganjila na
Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa
Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika
kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo
Mafunzo
haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike
kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya
kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa
Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia
namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake
Awamu
ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na
wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi
Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch
Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze
kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa
kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali
Pamoja
na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwana Mwanamke mmoja mwenye
mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa Lengo la
kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada
ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation
inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya
Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu
wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.
No comments:
Post a Comment