Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Ally Mwalimu akiingia katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) leo asubuhi kwa ajili ya kukagua utengenezaji
wa mashine ya MRI na CT- Scan.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiwa na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru leo asubuhi katika hospitali
hiyo.
Mtaalamu wa Mionzi kwenye chumba
cha mashine ya MRI, Job Joshua (kushoto) na Profesa Mseru (wa pili
kulia) wakimpatia maelezo Waziri Ummy Mwalimu (katikati) wakati
alipotembelea leo hospitali hiyo kukagua utengenezaji wa mashine hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora
Lwakatare akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Waziri kuhusu maendeleo ya
utengenezaji wa mashine ya MRI leo asubuhi.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Profesa Mseru kuelekea kwenye chumba cha X-ray cha digitali.
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora
Lwakatare (wa kwanza kulia) akimpatia maelezo mheshimiwa Waziri, Ummy
Mwalimu (katikati) kuhusu utengenezaji wa mashine hiyo leo asubuhi.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akizungumza leo asubuhi na wagonjwa wanaosubiri vipimo katika hospitali hiyo.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu
akiwa katika chumba cha CT-SCAN, huku Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora
Lwakatare akimpatia maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi wakati
ikiwa nzima.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akifafanua jambo baada ya kupewa maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment