RAIA HAO WA EPHIOPIA WAKIWA CHINI YA ULINZI MKALI
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE WILBROAD MUTAFUNGWA AKITOA TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
HUYU NI MIONGONI MWA MADEREVA DEREVA NI SALM MANGA WA MIKUMI
HAYA NI MAGARI AMBAYO WAHAMIAJI HARAMU AMBAO NI RAIA WA EPHIOPIA WALIKUWA WAKISAFIRISHWA
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Raia 29 wa Ethiopia Kwa Tuhuma za Kuingia na Kuishi Nchini Kinyume cha Sheria , Huku Likiwashikilia Raia Watatu wa Tanzania Ambao Walikuwa Wakiwasafirisha Raia Hao wa Ethiopia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbrod Mutafungwa Amesema Raia Hao Wamekamatwa Majira ya Saa Saba Usiku Disemba 14 Mwaka Huu Katika Barabara ya Dar Es Salaam Kuelekea Tunduma Eneo la Mji wa Makambao.
Mmoja wa Madereva Waliokuwa Wanawasafirisha Raia Hao wa Ethiopia Salim Manga Mkazi wa Mikumi Amesema Alipigiwa Simu na Rafiki Yake Ambaye Hakumtaja Jina Kuwa Kuna Watu Wako Eneo la Kitonga Wanatakiwa Kusafiri Kuelekea Harusini, .
Katika Hatua Nyingine Kamanda Mutafungwa Ameelezea Tukio la Mauwaji ya Thadei Mtengwa Mkazi wa Kijiji cha Msimbwa Kata Ya Luponde Aliyeuwawa Kwa Kuchomwa na Kitu Chenye Ncha Kali Sehemu za Tumboni Upande wa Kushoto na Watu Wasiofahamika .
Kamanda Mutafungwa Ametoa Wito Kwa Wananchi wa Mkoani Humo Kushirikiana na Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Kwa Toa Taarifa Zitakazofanikisha Kukamatwa Kwa Wahalifu wa Matukio Mbalimbali, na Kwamba Licha ya Jeshi Hilo Kuendesha Msako wa Kuwabaini Wahalifu , Wananchi Wanatakiwa Kuwa Makini Hasa Katika Kipindi Hiki cha Kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.
No comments:
Post a Comment