Dokta Mwele Malecela wa Kituo cha
Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya mahojiano jana na baadhi ya
vyombo vya habari vilivyoshiriki katika warsha ya siku mbili
inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa
ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa wa Ebola na mengineyo
katika bara la Afrika na kwingineko duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa
pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na
taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya
kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya
wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili
inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa
ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara
la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na
taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya
ya CORDS ya nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment