UGONJWA WA KIPINDUPINDU HAPA NCHINI
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na
ugonjwa wa Kipindupindu ulivyoweza kupungua ikiwa kukiwa na vifo vya
watu 493 kwa Tanzania Bara.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jamii.
JUMLA ya watu 493 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu Tanzania bara tokea ulipoibuka jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema kuwa jumla
ya watu 12,222 wameugua ugonjwa huo tangu ugonjwa huo wa mlipuko kuaza
hapa nchini.
“Ugonjwa
wa Kipindupindu umeanza tokea tarehe Desemba 15, 2015 katika mkoa wa
Dar es salaam na kusambaa katika mikoa 21 ya Tanzania” Mhe. Mwalimu
amesema.
Hata hivyo,Waziri huyo,amesema waathirika wa kipindupindu wameanza kupungua katika mikoa ya
Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.
Pia ameitaja Iringa na Kilimanjaro kuwa ni mikoa ambayo imeweza kuthibiti ugonjwa huo hatari.
Mwalimu akitoa takwimu za ugonjwa huo, amesema hivi sasa kuna
wagonjwa wapya 76, hivyo idadi ya wagonjwa wapya imefikia 493 na kifo
kimoja.
“Hadi sasa mkoa wa Morogoro vijijini unaongoza kwa wagonjwa 56,
ukifuatiwa na Arusha (28), Rorya (22), Bunda (21) na Kigoma vijijini
17.” Mhe. Mwalimu amesema”
Aidha Mhe.Mwalimu ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwa
ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwa barabarani,kuuza vyakula katika
mazingira yasiyo safi na salama,huku akitaka kuandaliwa kwa taarifa za
kila wiki kuhusu ugonjwa huo.
Akitoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa, kuwa walete taarifa
sahihi za mlipuko wa ugonjwa huo kwa ajili ya kuudhibiti. Na kwa
kuwasisitiza watanzania kunywa maji safi na salama na kunawa mikono kwa
maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment