RC
Makalla awashukuru wana Kilimanjaro kwa kujitokeza kwa wingi kufanya
usafi, ataka kila Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa usafi
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla, amewapongeza wakazi na
wananchi wake katika mkoa huo kwa kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli la kufanya usafi na
kutunza mazingira katika siku ya Uhuru, 9 Desemba iliyoadhimishwa jana
nchini kote.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla juu na chini mwenye
miwani akishiriki kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru,
yaliyoadhimishwa jana nchini kote.
Kwa kupitia siku hiyo, RC Makalla ameagiza wakazi wake na wananchi
kuitumia kila siku ya Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa ajili
ya mwendelezo wa kufanya usafi ili kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa
safi.
Akizungumza jana mkoani Kilimanjaro, RC Makalla alisema kwamba
wananchi wake walijitokeza kwa wingi kufanya usafi, huku akiwataka
waendeleze kasi yao ya kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa safi. Alisema
kwa kufanya hivyo si tu mkoa wao utakuwa safi, ila hata suala la
magonjwa ya miripuko linaweza kuwa hadithi kutokana na kutunza mazingira
yao. “Jana nilishirikiana kwa pamoja na wananchi wangu kufanya usafi,
huku nikifanya usafi soko la Memorial, Hospitali Mawenzi na Soko la
Marangu.
“Pamoja na kujitokeza huko kwa wananchi, naomba suala hili liwe
jadi yetu kuanzia ngazi ya kaya, mtaa, kitongoji na katika maeneo yote,”
alisema. RC Makalla aliagiza Halmashauri zote kuhakikisha masoko yote
yanakuwa safi na takataka zinazolewa kwa wakati, bila kusahau mitaro.
Click here to Reply, Reply to all or Forward 193.18 GB (15%) of
1,240 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 0 minutes
ago Details
No comments:
Post a Comment