MKESHA WA MWAKA MPYA KITAIFA KUFANYIKA VIWANJA VYA UHURU DESEMBA 31.
Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii.
MAASKOFU
na Wachungaji wa kamati ya maandalizi ya Mkesha wa mwaka mpya Kitaifa
kufanyika katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam Desemba
31,Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Askofu Godfrey Malassy,
wamewaomba watanzania wote kujitokeza siku ya Desemba 31 katika
kuliombea Amani na Utulivu wa Taifa letu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste ,
ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC),
Askofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
amesema kuwa lengo la Mkesha huu ni Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kutuvusha mwaka 2015 na kuupokea mwaka 2016 ikiwa ni pamoja na
mkumshukuru Mungu kwa kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu kwa amani na tuzidi
Kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe
Joseph Magufuli kwa kuongoza Taifa letu.
"Mkesha huu ni kwa watu wote na wakumshukuru Mungu na kutoa sadaka
,ambazo zitakusanywa na kupelekwa kwa watu wenye mahitaji maalum"
alisema Malassy.
Askofu Malassy aliongeza kuwa anamshukuru Mungu kwa kuandika
kitabu kinachoitwa IJUE SIRI YA AMANI KWA TAIFA,ambacho kinapatikana kwa
shilingi 5000, kwa lengo la kufunua asili, thamani na jukumu letu
katika kulinda Amani kwa kila Mtanzania bila kujali dini, itikadi,
ukabila na hata utaifa.
No comments:
Post a Comment