mwenyekiti wa serikali Ya Mtaa Wa Kibena Hospitali Winfred Kayombo Kupitia CHADEMA
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE WILBROAD MUTAFUNGWA AKITOA TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
HAPA NDIPO MTOTO HUYO ALIIBIWA NA KUPATIKANA MAKAMBAKO KATA YA MJIMWEMA
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linamshikilia Frola Msigwa Mwenye Umri wa Miaka 39 Mkazi wa
Mjimwema Makambako Kwa Tuhuma za Kumuiba Mtoto Alen Makweta Mwenye Umri wa Miezi
Mitatu Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe Iliyoko Eneo la Kibena.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi Iliyotolewa Kwa Vyombo Vya Habari na Kusainiwa na
Kamanda wa Jeshi Hilo Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Inasema Kuwa Tukio Hilo
Limetokea Decemba 16 Majira Saa Saba Mchana Katika Hospitali Hiyo,na Kwamba Mtuhumiwa
Amekamatwa Maeneo ya Makambako Akiwa na Mtoto Huyo.
Aidha Taarifa Hiyo Inaeleza Kuwa Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Dhidi ya Tukio Hilo na
Mara Uchunguzi Utakapokamilia Mtuhumiwa Atafikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma
Zinazomkabili, Huku Jeshi Hilo Likitoa Wito Kwa Kinamama Kuwa Makini Ikiwa ni Pamoja na
Kutowaachia Watoto Wao Watu Wasiowafahamu.
Upland's Redio Imezungumza na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibena Hospitali Winfred Kayombo
Ambaye Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Huku akiwasihi kina mama kuwa makini na malezi ya watoto wao ikiwemo kuwa nao karibu wakati wote .
Kwa Upande Wao Wazazi Wa Mtoto Aliyeibiwa Katika Eneo La Hospitali Ya Kibena
Wameushukuru Uongozi wa Mtaa Huo , Wananchi Pamoja na Jeshi la Polisi Kwa Kufanikisha
Kupatikana Kwa Mtoto Wao Huku Wakielezea Mazingira Alivyoibiwa.
Nao Baadhi ya Wananchi Waliozungumza na Kituo Hiki Wameiomba Serikali ya Mkoa wa Njombe
Kuboresha Mazingira ya Hospitali Hiyo Ikiwemo Ulinzi na Kujenga Uzio Ambao Utasaidia kuzuia
Matukio Kama Hayo Katika Hospitali Hiyo Kupungua.
No comments:
Post a Comment