Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, November 17, 2015

WANAFUNZI WA MIFUGO NA KILIMO WATAKIWA KUSOMA ZAIDI ILI KUWASAIDIA WAZAZI WAO

02-041
Wanafunzi atabibu wa Mifugo nchini Malawi wakipata mafunzo kutoka kwa Dk. Ruprecht Herbst wa taasisi ya  WTG ya Ujerumani nchini Malawi
………………………………………………………………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad Arusha
WANAFUNZI wa vyuo vya Mifugo Tengeru  Wilayani Arumeru na Laborsoit wilayani Simanjiro, wametakiwa kujifunza vitu vipya kila siku, iliwaweze kuwasaidia wazazi wao wakulima na wafugaji vijijini, ambaowamewasomesha.

Akizungumza jana katika kata ya Kikatiti, Afisa Mifugo na Uvuvi halmashauri ya Meru, Aman Sanga, katika mafunzo ya wiki moja ya ustawi wa wanyama, yaliyotolewa na shirika la Meru Animal Welfare Organization kwa kushirikiana na shirika la Ujerumani la WTG likiongozwa na jopo la wawezeshaji Dk. Ruprecht Herbst na Tina Lang,
kwa wanafunzi zaidi ya 20, aliwasisitiza kuzingatia mafunzo hayo ya nadharia na vitendo.
Alisema kuwa mtaalamu wa Mifugo ni mwanasayansi, hivyo lazima kila kukicha kuingiza ujuzi mpya kichwani ili kujisaidia mwenyewe kuongeza ujuzi zaidi na wafugaji, pamoja na wakulima, ili wafuge mifugo yenye
tija.

“Ili kuweza kupambana na magonjwa ni lazima mtaalamu husika uwe na ujuzi wa kutosha kichwani, kwani huwezi kutibu kwa kutumia vitabu, hivyo mafunzo haya ytawajenga sana na kuleta mabadiliko kwa
wafugaji,”alisema.
Naye Mratibu wa shirika la Meru Animal Welfare Organization, Johnson Lyimo, alisema wanatoa mafunzo hayo, ili  kuwafikia wanafunzi zaidi ya 20,000 kufikia mwaka 2018.

Alisema lengo kubwa la mafunzo hayo kuongeza ustawi wa wanyama katika jamii na kuongeza ujuzi kwa wataalamu wa mifugo nchini.

Johnson alisema kwa upande wa wanafunzi wanaopati wa mafunzo hayo, yatawasaidia watakapomaliza vyuo vyao watafanya kazi kwa ufanisizaidi.

“Japokuwa tunachangamoto kubwa ya kuendesha mafunzo haya kuwa endelevu
kwa sababu ya ukosefu wa fedha, kwani kunahitajika kuwe na vifaa vya
kutosha vitakavyotoa mafunzo kwa vitendo,”alisema.

Kwa upande wa mgeni mwalikwa toka shirika la Donkey Saltuary Kenya,Dk. Solomon Onyango, aliwasihi wanafunzi hao kuzingatia mafunzo hayo adimu, ili wapate ujuzi na ukawanufaishe jamii wanazotoka kwa ustawi wa wanyama.

Meneja Mipango wa Kimataifa toka shirika la WTG toka Ujerumani, Dk.Ruprecht Herbst, alisema kupitia shirika hilo ameweza kutoa mafunzo kwa vitendo na nadharia nchi 50 duniani na kote hutoa na vyeti iliviwasaidie kufahamika katika jamii zao.

“Naamini baada ya mafunzo haya, mtaweza kutibu wanyama na kusaidia jamii zenu mnazotoka,hivyo muhimu kuzingatia ili waweze kuwa wataalamu bora,”alisema.

No comments:

Post a Comment