Michuano ya Kombe la Shirikisho ya Azam Sports inafunguliwa rasmi Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa
kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam
itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Siku hiyo pia kutakuwa na mechi
kati ya Kariakoo ya Lindi na Changanyikeni FC ya Dar es Salaam
itakayochezwa kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wakati Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Wenda FC ya Mbeya na Madini SC ya Arusha.
Bingwa wa michuano hiyo
inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano
ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment