Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Ernest Mangu akizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Mkoa wa Mara
wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo jana.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Ernest Mangu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho
Stephen wakati walipokutana jana .IGP yupo katika ziara ya kikazi katika
mkoa huo kukagua utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe.
Zeletho Stephen akizungumza katika kikao cha wadau wa amani mkoani
Mara.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye
ndiye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho wakati alipokuwa katika
ziara ya kikazi katika mkoa huo.
Baadhi ya wadau wakichangia mawazo
katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara kilichohudhuriwa na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni
rasmi wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
…………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wadau wa Amani mkoani Mara
wamemhakikishia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu
kuendelea kuitunza amani na kuimarisha usalama katika mkoa huo hasa
kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwa kuna maisha baada ya
uchaguzi.
Waliyasema hayo wakati
walipokuwa wakitoa maoni yao wakati wa kikao kilichohudhuriwa na wadau
mbalimbali wa amani mkoani humo wakiwemo Wanasiasa, Viongozi wa
Uchaguzi, Wagombea, Asasi za kiraia, Viongozi wa dini, Wazee wa kimila
na Viongozi wa dini mkoani humo.
Walisema mkoa huo umekuwa shwari
hasa baada ya kuundwa kwa Kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime na rorya
hivyo wananchi wote hawana budi kuendeleza juhudi za Jeshi la Polisi kwa
kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unaenda salama mkoani humo.
Akizungumza katika kikao hicho
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ameahidi Jeshi la
Polisi kutoa ushirikiano wa kutosha na kusimamia vyema uchaguzi ili
kuhakikisha kila mwananchi anashiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu
bila kutishwa na wahalifu.
Alisema Tume ya Uchaguzi imeweka
utaratibu mzuri wa kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo hivyo
hakuna haja ya wafuasi kukaa nje ya vituo vya kupigia kura kwa
kisingizio cha kulinda kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kujenga mazingira
ya kuleta vurugu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma,
Mhe,Zeletho Stephen alisema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari
hivyo ni jukumu la kila mdau kuhakikisha anashiriki kwa nafasi yake
kuimarisha usalama na amani hasa katika kipindi hiki.
IGP Mangu yupo katika ziara ya
kikazi katika mkoa wa Mara kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Jeshi
la Polisi ambapo pia amekuwa akitumia fursa hiyo kukutana na wadau
mbalimbali ili kushauriana jinsi ya kuimarisha amanai na usalama katika
maeneo yao
No comments:
Post a Comment