Mgombea Ubunge Jimbo La Njombe Kusini Kupitia Chama Cha ACT Wazalendo Emilian Msigwa Ameahidi Kuboresha Uchumi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Na Kutoa Ajira Kwa Vijana Kupitia Mradi Wa Mabwawa Ya Samaki Ambayo Atakwenda Kuanzisha Endapo Wananchi Watampatia Ridhaa Ya Kuongoza.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mgombea Ubunge Emilian Msigwa Wakati Wa Muendelezo Wa Kampeni Zake Akiwa Kijiji Cha Utengule Ambako Ameahidi Kuondoa Umasikini Kwa Wananchi Kwa Kutoa Mbinu Mbadala Za Maendeleo Ya Kila Mwananchi Ikiwemo Kushawishi Kujiunga Kwenye Vikundi Na Kupata Mikopo Kwenye Tasisi Za Kifedha.
Bwana Msigwa Amesema Kuwa Endapo Wananchi Watampa Ridhaa Ya Kuongoza Jimbo La Njombe Kusini Hatua Ya Utekelezaji Wa Miradi Ya Halmashauri,Kata Na Vijiji Atahakikisha Unafuata Misingi Na Kanuni Za Kisheria Ikiwemo Kuwapunguzia Michango Wananchi Ambao Walibebeshwa Mzigo Mkubwa Na Halmashauri Ya Mji Wa Njombe.
Swala La Miundo Mbinu Ya Barabara Za Kuunganisha Vijiji Mbalimbali Amesema Ataipa Kipaumbele Ambapo Baadhi Ya Majukumu Alikwisha Anza Kutekeleza Kabla Ya Kugombea Nafasi Ya Ubunge Jimbo La Njombe Kusini Ikiwemo Kusomesha Baadhi Ya Watoto Yatima Pamoja Na Kuboresha Miundombinu Ya Barabara.
Kwa Upande Wake Wananchi Wa Kijiji Cha Utengule Wameshukuru Kwa Kufika Na Kutoa Ahadi Hizo Na Kusema Kuwa Emilian Msigwa Wanamufahamu Kama Mtoto Wa Nyumbani Kwao Na Kuahidi Kumpatia Kura Za Kishindo Ifikapo Octoba 25 Mwaka Huu Huku Wakimpongeza Kwa Jitihada Za Kusomesha Watoto Yatima Na Wasiyojiweza.
No comments:
Post a Comment