Na Francis Godwin Iringa

Taarifa
iliyotolewa na Ofisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso ametanabaisha kuwa, madawati hayo
yaliyotengenezwa kwa kuzingatia umri wa wanafunzi, yatasambazwa katika
shule 10 za msingi wilayani humo.
Aidha,
Mwakapiso imevitaja vigezo ilivyotumika kutoa kipaumbele katika shule
hizo kuwa ni pamoja na mgawavyo wa majimbo na halmashauri, uhaba wa
madawati uliopo kwa kila shule sanjari na kigezo cha upya wa shule
husika, ambapo halamashauri ya wilaya yenye shule 144 na majimbo 02
imepata madawati 320 kwa shule 8 huku Halmashauri ya mji wa Mafinga
yenye shule 33 na jimbo moja ikipata madawati 80 kwa shule 02.
Shule
zilizonufaika na madawati hayo kwa wilaya ya Mufindi ni shule za msingi
Ikweha., Kipanga “A”, Ilasa, Igomaa na Mlimani nyingene ni Nzivi,
Ihegela na Sawala, wakati halmashauri ya mji Mafinga ni shule mpya ya
msingi Mwongozo na shule ya msingi Kilimani.
.//////////////////////////////////MWISHO/////////////////////////
No comments:
Post a Comment