MGENI RASMI AKIKABIDHI VYETI KWA BAADHI YA WAZEE WALIOHUDHURIA SEMINA HIYO WA KUTOKA WILAYA ZA MAKETE,LUDEWA,WANGING'OMBE NA NJOMBE
WENGINE NI WATUMISHI WA SERIKALI WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO YA WAZEE
MGENI RASMI AFISA UTUMISHI MKOA WA NJOMBE JAFARI SIMIKA ALIKWENDA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PADI TANZANIA ISKAKA MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAZEE WALIOHUDHURIA SEMINA HIYO.
HAWA NI WAZEE WAKIWA KWNYE PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI PAMOJA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PADI TANZANIA ISKAKA MSIGWA
Na Michael Ngilangwa
Serikali Imekili Kuwepo Kwa Changamoto Kubwa Inayowakabili Wazee Ya Kukosekana Kwa Mitaji Ya Kuendeshea Shughuli Za Uzarishaji Mali Na Kusababisha Kujikuta Wakiishi Katika Mazingira Magumu Na Kukosa Mahitaji Muhimu Katika Maeneo Mbalimbali Hapa Nchini Ikiwemo Njombe
Kauli Hiyo Imetolewa Na Afisa Utumishi Mkoa Wa Njombe Jafari Simika Akiwa Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi Wa Semina Ya Siku Moja Iliyofanyika Kwenye Ukumbi Wa Milima Motel Mjini Njombe Na Kusema Kuwa Tatizo La Kukosa Huduma Za Afya Nayo Changamoto Kwa Wazee.
Aidha Bwana Simika Amesema Kuwa Wazee Wamekuwa Wakikabiliwa Na Tatizo La Uduni Wa Huduma Za Afya Umesababisha Wazee Wengi Kuingia Kwenye Wimbi La Umasikini Kutokana Na Kipato Wanachokipata Kutumika Kwenye Matibabu, Janga La Ukimwi Linawapa Mzigo Wa Kutunza Wajukuu.
Bwana Simika Amesema Serikali Inaendelea Kuboresha Huduma Za Afya Kwa Wazee Na Walemavu Kwa Kushirikiana Na Mashirika Mbalimbali Na Kuwataka Wadau Kuunga Mkono Jitihada Za Shirika La PADI Kuwawezesha Wazee Kupitia Halmashauri Zao Ili Kuinua Uchumi Kwa Wazee Hao.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Shirika La PADI Tanzania Bwana Iskaka Msigwa Amesema Kuwa Shirika Hilo Limeamua Kuvisajili Vikundi 24 Ambavyo Vimepatiwa Vyeti Vyao Kwa Lengo La Kuwasaidia Wazee Kupata Misaada Mbalimbali Kutoka Kwa Wadau Wengine.
Bwana Msigwa Amesema Kuwa Kwa Muda Wa Miaka 15 Wamekuwa Wakitoa Fedha Kutoka Kwa Wafadhili Huku Jitihada Za Kuvisajili Vikudi Vingine Zikiendelea Kadri Inavyowezekana Ambapo Kupitia Usajili Huo Utasaidia Taasisi Zingine Za Kifedha Kuwasaidia Mikopo.
Wakizungumza Mara Baada Ya Kukamilika Kwa Semina Hiyo Baadhi Ya Washiriki Wamesema Kuwa Wanashangazwa Na Viongozi Ambao Wanapuuza Sera Ya Wazee Ya Kuthaminiwa Na Kupatiwa Huduma Mbalimbali Zikiwemo Za Matibabu Bure Ambayo Hadi Sasa Utekelezaji Sifuri.
No comments:
Post a Comment