

Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Jana Amepokea Mwenge Wa
Uhuru Kutoka Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Amina MaSenze Ambao Baada
Ya Kupokelewa Katika Mtaa Wa Kipagamo Ulitembelea Na Kuzindua
Miradi Mbalimbali Ya Halmashauri Ya Mji Wa Makambako Ikiwemo Nyumba
Tano Za Watumishi Wa Makambako.
Akipokea Mwenge Huo Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Amina Masenza, Mkuu
Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amesema Mwenge Huo Kwa Mkoa
Wa Njombe Utatembelea,Kuzindua Na Kuweka Mawe Ya Msingi Kwenye
Miradi 45 Yenye Thamani Ya Zaidi Ya Shilingi Bilioni 13 Na
Utakabidhiwa Julai Mosi Mkoani Mbeya Huku Mkoani Iringa Ukiwa
Umekimbizwa Kilomita 622 Na Kupitia Miradi 35 Yenye Thamani Ya
Shilingi Bilioni 4.
Miradi Mingine Iliyozinduliwa Na Kutembelewa Na Mwenge Huo Ni
Pamoja Na Bweni La Wasichana Na Nyumba Ya Walimu Katika Shule Ya
Sekondari Maguvani,Kuzindua Daraja La Kijiji Cha Ilengititu,
Zahanati Ya Kichiwa Na vyoo Vya Shule Ya Msingi Kichiwa Na Mradi
Wa Maji Katika Kijiji Cha Kifumbe.
Akizungumza Wakati Wa Kuweka Mawe Ya Msingi Katika Miradi Wa
Surplise Beach Na Maabara Ya Shule Ya Sekondari Sovi, Kiongozi Wa
Mbio Za Mwenge Kitaifa Kwa Mwaka 2015 Juma Khatibu Chum Amesema
Serikali Inatambua Uwepo Wa Taasisi Za Watu Binafsi Pamoja Na
Jitihada Zinazofanywa Na Wananchi Katika Kutekeleza Miradi Kwa
Manufaa Yao Na Kutaka Jitihada Hizo Kuendelezwa.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Mradi Wa Kukuza Uchumi Na Utunzaji
Wa Mazingira Wa Beach Surplise Patrick Alex Kyando Amesema Mradi
Huo Utakapo kamilika Unatarajia Kutoa Ajira Kwa Vijana Zaidi Ya 178
Ambapo Kwa Sasa Umegharimu Jumla Ya Shilingi Milioni 605 Na
Unatarajia Kugharimu Bilioni Mbili Na Milioni 17 Hadi Kukamilika
Kwake Mwezi Decemba 2018.
No comments:
Post a Comment