Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, June 7, 2015

Mkuu wa wilaya ya Mufindi amewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuwa walinzi namba moja dhidi ya wenyetabia ya kuharibu mazingira




Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA amewataka wakazi wa mkoa wa

Iringa kuhakikisha wanakuwa walinzi namba moja dhidi ya watu wenyetabia ya

kuharibu mazingira katika maeneo yao, kwani kwa kutofanya hivyo ni sawa na

kujiuwa wenyewe.



Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya habari na mawasiliano ya Halmashauri ya wilaya ya

Mufindi Imetanabasha kuwa, mkuu wa wilaya ameyasema hayo kwenye kilele cha

siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Vikula Wilayani

Mufindi Mkoani Iringa alipomwakilisha mkuu wa Mkoa kama mgeni rasmi.



MHITA amesema endapo wananchi hawata chukua hatua dhidi ya watu wenye

tabia ya za kuvuna miti kiholela, ufugaji wa mifugo usiozingatia taratibu za

kitaaluma, uchomaji moto ovyo, uharibifu wa vyanzo vya maji, uwindaji haramu

na ukataji mijti ovyo, kunauwezekano mkubwa wa kutoweka kwa misitu na

vyanzo vya maji nchini na kuhatarisha ustawi wa mwanadamu.




Aidha, ameyataja madhara yanayotokana na uharibifu wa mazingira kuwa ni

pamoja na mbadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa hewa ya ukaa, misitu

kuteketea kwa moto, kupungua kwa kiasi cha mvua na majra yake kubadilika

kuongezeka kwa joto sanjari na kupungua kwa mavuno mashambani.

Kaulimbiu ya siku ya mazingira mwaka huu inasema ndoto bilioni saba. Dunia moja . Tumia rasilimali kwa uangalifu.

No comments:

Post a Comment