Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, June 5, 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA YAFANYIKA LEO KWA WILAYA YA NJOMBE YAMEFANYIKIA MATIGANJORA


 NGOMA YA ASILI IKIBURUDISHA KWA UZURI KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA SERIKALI YA KIJIJI HICHO MWENYE MZURA HUYO ANAITWA KASUTI
 








 MTI UMEKWISHA KUPANDWA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA





 NGOMA YA ASILI IKIBURUDISHA LEO










 KAIM MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE BI.ELITA MLIGO AKISOMA RISALA FUPI KWA MGENI RASMI

MWENYE KOTI JEUPE NI MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE  SARAH DUMBA


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Amekabidhi Zawadi na Vyeti Vya Utunzaji na Usafi wa Mazingira Kwa Kata za Ikuna na Kidegembye Kwa Kufanikiwa Katika Utunzaji na Usafi  wa Mazingira.

Akizungumza Mara Baada ya Kukabidhi Vyeti na Zawadi Hizo Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Yaliyofanyika Kiwilaya Katika Kijiji cha Matiganjora, Bi. Dumba Amewataka Wananchi Kuendelea Kutunza Mazingira na Kuacha Tabia ya Kuchoma Moto Ovyo.

Nao Baadhi ya Wananchi Walioshiriki Maadhimnisho Hayo Wamesema Licha ya Kuaadhimisha Siku Hiyo Lakini Bado  Wanakabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukosefu wa Maji Safi na Salama Pamoja na Elimu ya Matumizi ya Vyoo Bora.

Awali Akisoma Risala Kwa Mgeni Rasmi Kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Bi. Elita Mligo Amesema Halmashauri Hiyo Inaendelea Kuwaelimisha Wananchi Katika Utunzaji na Usafi wa Mazingira.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Huadhimishwa Mei 5 Kila Mwaka Ambapo Kwa Mwaka Huu Maadhimisho Hayo Kitaifa Yameadhishwa Mkoani Tanga Chini ya Kauli Mbiu Inasemayo ''NDOTO BILION SABA,DUNIA MOJA,TUTUMIE RASILIMALI  KWA UANGALIFU''.

No comments:

Post a Comment