Diwani Wa Kata Ya Mjimwema Jimmy Ngumbuke Amewataka Wananchi Wa
Kata Ya Mjimwema Kuondoa Itikadi Za Kisiasa Katika Kusaidiana
Kwenye Matatizo Mbalimbali Ambayo Yamekuwa Yakijitokeza Ikiwemo
Kusaidia Wagonjwa Wanapoumwa Ili Kudumisha Umoja Na Mshikamano
Katika Maisha Ya Kila Siku.
Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Tukio La Wizi Wa Mtoto
Katika Mtaa Wa Mjimwema Diwani Ngumbuke Amesema Kuwa Matatizo Hayo
Yanatokana Na Wananchi Wa Mtaa Huo Kuwa Na Itikadi Za Kisiasa
Ambazo Zinasababisha Umoja Kutokuwepo Jambo Ambalo Amesema Wakati
Wa Kutekeleza Majukumu Ya Serikali Itikadi Zinatakiwa Kuondolewa Na
Kuwa Kitu Kimoja.
Aidha Bwana Ngumbuke Amesema Kuwa Wananchi Wanapaswa Kuwalinda
Watoto Kama Watoto Wao Huku AKitaka Kufuata Maadili Yenye Kujenga
Na Kutaka Kuwasaidia Wagonjwa Katika Kuwachangia Michango Ili
Mgonjwa Apone Na Kuendelea Na Majukumu Ya Kitaifa Kama Ilivyokuwa
Hapo Zamani.
Bwana Ngumbuke Amesema Kuwa Kwa Sasa Wananchi Wengi Wamekuwa
Wakithamini Kuchangia Kwenye Misiba Na Siyo Ugonjwa Ambapo Ndugu
Wengi Wamekuwa Wakipoteza Maisha Kwa Kukosa Dawa Ya Shilingi Elfu
Kumi Na Nauri Ya Usafiri Hususani Wakazi Wa Vijijini Ambako Ni
Mbali Na Eneo La Huduma.
Bwa Ngumbuke Amesema Kuwa Juzi Kuna Dada Mwingine Alitaka Kutapeli
Mtoto Katika Kituo Cha Afya Cha Njombe Mjini Baada Ya Dada Mmoja
Aliyekwenda Kupata Matibabu Kuombwa Amuachie Mtoto Kwa Kuwa Mwenye
Mtoto Alikuwa Anataka Kuingia Kwa Daktari Wakati Mtoto Akilia Na
Ndipo Aliposhitukiwa Kwamba Ni Mama Tapeli Ndipo Alipotokomea
Kusiko Julikana.
No comments:
Post a Comment